Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kutetea kiti chake cha Udiwani
katika kata ya MLETELE iliyopo katika manispaa ya SONGEA Mkoani RUVUMA baada
Mgombea wa kiti hicho MAURUS LUNGU kwa tiketi ya CCM kushinda katika uchaguzi
mdogo uliofanyika leo.
Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo
mdogo, msimamizi wa Uchaguzi huo ZAKARIA NACHOA amesema MAULUS LUNGU amepata
kura 955 akiwapiga mweleka Mgombea wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA
LEOCARDO MAPUNDA aliyepata kura 297, Mgombea SALUM CHALE wa Chama Cha Wananchi
CUF aliyepata Kura 27.
Uchaguzi huo umefanyika kwa lengo la
kuziba nafasi ya aliyekua diwani wa kata hiyo FLAVIAN LEGELE ambaye alifariki
Dunia
Hata hivyo Uchaguzi Mdogo wa kata ya
MLETELE uliingia doa siku moja kabla ya siku ya Uchaguzi baada ya wafuasi wa
Vyama viwili vilivyokua na upinzani Mkubwa CHADEMA na CCM kushambuliana kwa
mapanga ambapo watu sita wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa
Mjini SONGEA kwa Matibabu
Miongoni mwa waliojeruhiwa na
kulazwa Hospitali ni NYENJE ALLY MPONJI (32), MASHAKA MBAWALA (45) na THABIT
SULEIMAN (29) waliojeruhiwa kichwani mikononi na miguuni.
Wengine ni Mwenyekiti wa CHADEMA
Mtaa wa Changarawe aliyeshambuliwa kwa kipigo na majeruhi wengine walitibiwa na
kuondoka.
Chanzo cha vurugu hizo ni wafuasi wa
vyama hivyo kukutana katika eneo la kanisani na kisha kuanza kushutumiana na
ndipo mashambulizi yakaanza katika gari mojawapo lililokuwepo eneo la tukio na
ndipo mapigano yalipoanza na haikujulikana silaha aina ya mapanga, fimbo, mawe
na magongo yalikotoka na kuanza kutumika katika mapigano hayo
No comments:
Post a Comment