Katika kuonyesha
kuwa chama cha mapinduzi (CCM) hakikubaliki katika kata ya Mlangali
wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ni baada ya wapiga kura wa kata hiyo
kumgalagaza vibaya mgombea wa Chama cha mapinduzi (CCM) Bw.Andrew Mhagama
aliyewahi kukitumikia chama hicho kama katibu wa chama kwa wilaya mbalimbali
nchini na baadae kustaafu na kumchagua mgombea wa Chadema Faraja Mlelwa.
Uchaguzi huo umefanyika ni baada
ya eliyekuwa Diwani Bw.Kacheche kufariki dunia kwa kujinyonga kwa kamba
chumbani kwake kwa sababu zisizo fahamika mwanzoni mwa mwaka 2012.
katika uchaguzi huo
mgombea wa Chadema Bw Faraja ameshinda kwa tofauti ya kura 163 dhidi ya
mgombea wa CCM mzee Mhagama na hoja kubwa ya kufanya wapiga kura
kutomchagua Mhagama ni kuwa ni mzee ambaye itakuwa vigumu kufanyakazi na
mbunge wa jimbo hilo Deo Filikunjombe (CCM) ambae ni kijana.
Awali katika kampeni za mwaka 2010
Bw.Filikunjombe ambate ni mbunge wa jimbo la ludewa alinukuriwa na wananchi hao
akisema”nipeni mimi kura zote kwani ni kijana na kijana anaweza kufanyakazi
zaidi yam zee”,Mzee ambaye alikuwa ni mpinzani wake Prf.Mwalyosi.
Hivyo hata kampeni za kumsaidia
Mhagama Bw.Filikunjombe alikutana na maswali mengi kutoka kwa wananchi wake
yakumuuliza kwanini aliwaletea mzee wakati katika kampeni zake alisisitiza
wachaguliwe vijana ili walete mabadiriko
ya kimaendeleo.
Bw.Filikunjombe alionekana
kushikwa na kigugumizi na kuwataka wananchi kumchagua mzee huyo ili kuweka
uwiano ndani ya chama cha mapinduzi kwani wazee ni washauri wakuu ndani ya
chama chao.
“Kunichagua mimi kama kijana
isiwe fimbo kwa wengine tutambue wazee ndio washauri wetu wakubwa hivyo kama
madiwani wetu watakuwa vijana na wazee utendaji kazi utakuwa mkubwa kutokana na
ushauri watakaoupata vijana kutoka kwa wzeee”,alisema Filikunjombe katika
kampeni hizo.
Hata hivyo wananchi wa kata ya
Mlangali walionekana kutoridhishwa na majibu ya mbunge wao na kubaki na msimamo
wao wa kuchagua kijana ambaye ataendana kiutendaji kazi na Bw.Filikunjombe
ambaye ni kijana.
Msimamizi wa uchaguzi wa kata
hiyo Bw.Broun Kilanga alimtangaza mgombea wa CHADEMA kuwa mshindi na ndiye
atakayekuwa Diwani mpya wa kata hiyo kwani alimsinda mpinzani wake kwa zaidi ya
kura 163.
Bw.Mlelwa ameweza kuibuka mshindi
kutokana na sababu za kuwa kijana mdogo mwenye elimu kubwa kwani ana shahada
mbili hivyo kampeni zao na mwenendo wa uchaguzi mzima ulikuwa wa huru na haki
pia amani ilitawala katika mikutano mbalimbali ya kampeni zao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment