matunda ya Parachichi yakiwa yamevunwa tayari kwa kuingia sokoni
Mkuu wa
wilaya ya Ludewa Mh.Andrea Tsere akiwa katika picha ya pamoja na
wakulima wa mtandao wa kilimo cha Parachichi wilayani Ludewa na viongozi
wa mtandao huo mkoa wa Njombe.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Andrea Tsere akiwa katika picha ya pamoja na wakulima wa mtandao wa kilimo cha Parachichi wilayani Ludewa na viongozi wa mtandao huo mkoa wa Njombe.
Mratibu wa mtando wa wakulima wa Parachichi mkoa wa Njombe Bw.Erasto Ngole
Zao la Parachichi wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe limeanza kuleta neema kwa wakulima kwa kuwapatia kipato kutokana na zao hilo kuuzwa kwa bei kubwa kwani kilo moja imefikia shilingi 1500 hadi 2000 na kuwa na wateja wengi kutoka nchi mbalimbali.
Akitoa taarifa ya zao hilo katika kikao cha mtandao wa wakulima wa kilimo cha parachichi kilipofanyika wilayani Ludewa katika kata ya Mlangali mratibu wa mtandao huo mkoa wa Njombe Bw.Erasto Ngole alisema kuwa zao hilo ni dhahabu ya wakulima.
Bw.Ngole alisema kuwa wakulima wa parachichi Mkoa wa Njombe hususani wilayani Ludewa wameanza kuona umuhimu wa zao hilo ikiwa tofauti na mazao mengine kwani baadhi yao wanamiliki magari kutokana na kilimo cha parachichi hivyo ni zao linalowakomboa wakulima.
Alisema kuwa bado parachichi haitochi kwa wanunuzi kwani kumekuwa na makampuni mengi yanayohitaji zao hilo kwa wingi lakini uzarishaji bado uko chini hali inayowafanya wanunuzi hao kugombalina na wakati mwingine hutaka kutoa rushwa kwa uongozi wa mtandao ili wauziwe kampuni fulani na si vinginevyo.
Bw.Ngole aliwataka wakulima wa parachichi kuwaelimisha wakulima wa mazao mengine kulima zao la parachichi kwani wanunuzi hununulia shambani moja kwa moja tofauti na mazao mengine na hata uchumaji mkulima hahusiki bali huhusishwa wakati wa upimaji tu na si vinginevyo.
Alisema kwa wilaya ya Ludewa ni mkulima mmoja tu ndiye aliyeongoza kwa mauzo kwa mwaka 2017 kwani ameuza tani 23 na amepata zaidi ya shilingi milion 50 aliongeza kuwa zao hilo lipo la muda mfupi ambalo huanza kuchumwa kuanzi mti ukiwa na umri wa mika mitatu na kuendelea hivyo ni fulsa mpya kwa wakulima.
Akifungua mkutano huo wa mtandao wa wakulima wa Parachichi wilayani Ludewa Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Andrea Tsere aliwapongeza wakulima wa parachichi wilayani Ludewa kwa kuanzisha kilimo cha parachichi chenye manufaa makubwa katika jamii.
Mh.Tsere alisema kuwa kwa wilaya ya Ludewa hasa katika tarafa za Mlangali,Liganga na Mawengi parachichi ni zao ambalo litaleta ukombozi mkubwa kwa wakulima lakini katika tarafa za Mwambao na Masasi zao la Korosho linaendelea vizuri kutokana na uhamasishaji mkubwa uliofanyika.
Alisema kuwa alitoa agizo mwaka 2016 kila shule ya msingi na Sekondari kuwa na Nusu ekali ya zao la Parachichi hivyo hata yeye ni mdau mkubwa na tayari amejaribu kupitia baadhi ya shule na ameona agizo lake nimefanyiwa kazi hivyo aliwaagiza watendaji wa vijiji wote kuhakikisha kila shule inaongeza mashamba ya zao la Parachichi.
"nawaagiza watendaji wote wa vijiji kuwahamasisha wananchi kulima parachichi na kila mwananchi anatakiwa kuwa na ekali mbili ya zao hili ambalo mwisho wa siku ni ukombozi ndani ya familia kwa kujiongezea kipato pia shule zote zihakikishe zinaokeza ukubwa wa mashamba na kuwa na ekali walu moja kila shule ili kuepukana na utegemezi wa kuomba misaada",alisema Mh.Tsere.
mwisho
No comments:
Post a Comment