Mkurugenzi wa shirika la PADECO Bw.Willbad Mwinuka akiongea na wananchi wa kata ya Ludewa katika viwanja vya shule ya Sekondari Chief Kidulile
Wataalamu wa Ardhi na Ujenzi kutoka osifi za Halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakionesha ramani ya majengo ya Mabweni hayo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa na Diwani wa kata ya Ibumi Mh.Edward Haule akiongea na wananchi wa kata ya Ludewa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa na Diwani wa kata ya Ibumi Mh.Edward Haule akiongea na wananchi wa kata ya Ludewa
Mkurugenzi wa shirika la PADECO Bw.Willbad Mwinuka akiongea na wananchi wa kata ya Ludewa katika viwanja vya shule ya Sekondari Chief Kidulile
Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monica Mchilo akiwaelekeza wananchi namna ya ujenzi huo utakavyofanyika na nini kinahitajika kutoka kwa wananchi wake.
Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monica Mchilo akiwaelekeza wananchi namna ya ujenzi huo utakavyofanyika na nini kinahitajika kutoka kwa wananchi wake.
mtaalamu kutoka ofisi ya Ardhi Bw.Mgina akielekeza namna ya mejengo yatakavyokaa
Picha ya pamoja
wananchi wakifuatilia mkutano huo wa makabidhiano ya eneo la ujenzi na mipango mingine ya kukamilisha ujeni wa mabweni hayo.
wananchi wakifuatilia mkutano huo wa makabidhiano ya eneo la ujenzi na mipango mingine ya kukamilisha ujeni wa mabweni hayo.
Shirika
lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu mkoani Njombe la PADECO(participatory
Develompent Concern)ambalo ni shirika linalojihusisha na maendeleo shirikishi
katika jamii limeanza rasmi ujenzi wa mabweni mawili katika shule ya sekondari
Chief Kidulile iliyoka kata ya Ludewa ili kutatua changamoto zinazowakabili
wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Akikabidhiwa
eneo la kujenga mabweni hayo Mkurugenzi mtendaji wa Padeco Bw.Willbad Mwinuka
alisema kuwa shirika lake limekuwa likifanya kazi nyingi za kimaendeleo ndani
ya mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na wafadhiri mbalimbali pamoja na Jimbo
Katoliki la Njombe,hivyo kwa kata ya Ludewa shule ya Chief Kidulile itajengewa
mabweni mawili ambayo moja litakuwa kwaajili ya wanafunzi wa kike na jingine
kwaajili ya wanafunzi wakiume.
Bw.Mwinuka
alisema kuwa shirika lake linajihusisha na ujenzi wa miradi mbalimbali ambayo
ni changamoto kubwa kwa wananchi hivyo katika kata ya Ludewa Diwani wa kata
Mh.Monica Mchilo kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri,Mkuu wa wilaya
pamoja na ofisi ya Mbunge waliweza
kuwasilisha changamoto hiyo iliyokuwa kikwazo cha elimu kwa wanafunzi wa shule
ya Sekondari ya Chief Kidulile kwani richa yakuwa shile hiyo imekuwa na
wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita lakini kuna mabweni mawili
tu.
Alisema hali
hiyo iliwafanya wanafunzi kubanana lakini wengine kushindwa kuishi bwenini na
kuwalazimu kupanga katika nyumba vya mitaani ambapo ni hatari sana hasa kwa
wanafunzi wa jinsia ya kike kwani mtaani kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuwa
ni kikwazo katika masomo yao lakini kwa ujenzi wa mabweni hayo ya kisasa
utawapa fulsa wanafunzi kuishi katika
mazingira ya shule na kupata muda mwingi wa kujisomea.
Akikabidhi
eneo hilo la ujenzi wa mabweni ya kisasa Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monica
Mchilo alisema Kuwa mabweni hayo ni kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa kata
ya Ludewa kutokana na hali halisi hasa nyakati za mvua watoto wanafunzi wengi
hushindwa kuhudhuria masomo kutokana na umbali wa shule na wanakoishi,hivyo ni
kama miujiza ya mwenyezi Mungu kuwaleta PADECO ili kuwasaidia wanafunzi hao.
Mh.Monica
alisema kuwa richa ya kupata wafadhiri hao katika ujenzi wa Mabweni lakini
wananchi wa kata hiyo wanatakiwa kujitolea katika maandalizi ya mchanga na
tofari lakini mawe yamekwisha andaliwa kwani mfadhili atalipia mafundi,ujenzi
wote na vifaa vya viwandani lakini mahitaji yanayowezekana yanatakiwa
kuandaliwa na wananchi wenyewe.
“Naomba wananchi
tushirikiane hii ni bahati iliyoje kwetu kwani kunashule nyingi wilayani hapa
ambazo hazina mabweni lakini sisi tumepata bahati hivyo naomba tuitumie
kikamirifu ili kuwafanya wafadhiri hawa wasihame kata hii na kwenda kata
nyingine,na naomba wakimaliza ujenzi huu wanaweza kutusaidia kutatua changamoto
ya maji safi na salama”,alisema Mh.Monica.
Aidha
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Ludewa ambaye pia ni Diwani wa kata ya
Ibumi Mh.Edward Haule aliushukuru viongozi wa PADECO hasa Mkurugenzi Bw.Mwinuka
kwa kuiangalia wilaya ya Ludewa kwa jicho la pekee kwani tayari shirika hilo
limeshatekeleza miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Ludewa na
imekamilika vizuri ambapo imepunguza changamoto baadhi zilizokuwa zikiwakabili
wananchi wa wilaya ya Ludewa.
Mh.Haule
alisema kuwa ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa,Mkuu wa
wilaya pamoja na ofisi ya mbunge wa Jimbo la Ludewa itahakikisha mradi huo
unakamilika kwa wakati ili kuwatia nguvu wafadhiri waweze kuendelea kuifadhiri
wilaya ya Ludewa katika miradi mbalimbali hivyo mkurugenzi wa PADECO aondowe
wasiwasi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment