Uongozi na bodi ya shule ya Morning Star ukiwa katika picha ya pamoja shuleni hapo
Kaimu Mkurugenzi wa Morning Star Bw.Augustino Mwinuka akiwa Ofisini kwake.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa shule ya Morning Star Bw.Augustini Mwinuka akiwa ameshika chati cha usajiri wa shule hiyo.
Uongozi na bodi ya shule ya Morning Star ukiwa katika picha ya pamoja shuleni hapo
Uongozi wa
shule ya watoto wadogo ya Morning star
iliyoko wilayani katika mkoa wa Njombe imewataka wazazi wilayani Ludewa kujenga
utamaduni wa kuwapeleka watoto wadogo shule na kuachana na mazoea ambayo
yalizoeleka kuwa ni lazima mtoto afikie umli wa kwenda shule ya awali.
Hayo yamesemwa
leo na kaimu mkuregenzi mtendaji wa shule ya watoto ya Morning star Bw.Augustino Mwinuka wakati
akiitamburisha namba ya usajiri ya shule hiyo kwa viongozi wa bodi ya shule na
baadhi ya wazazi walipofika shuleni hapo kushuhudia namba hiyo ya usajiri wa
shule ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wakazi wa wilaya ya Ludewa.
Bw.Mwinuka
alisema kuwa baadhi ya wazazi wilayani Ludewa wamekuwa na tamaduni ya zamani ya
kuwapeleka watoto wao katika shule za awali za Serikali na kutowapeleka katika
shule za watu binafsi ambazo nazo hutoa elimu bora kwa kuhofia usajiri wa shule
hizo,hivyo ni wakati muafaka kwa wazazi kuitumia shule ya Morning Star ambayo
ambayo tayari usajiri wake umekamirika.
Alisema kuwa
shule hiyo imeshapata usajiri wa no.IR.05/3/EA.002 kwa shule ya awali na
IR.05/3/002 kwa shule ya msingi na imesajiriwa kwa jina la Morning star ikiwa
na mkondo mmoja kwani shule hiyo ni ya kutwa na Bweni hivyo wazazi wanapaswa
kutumia fulsa hii kwani ni shule pekee ya Binafsi iliyosajiriwa wilaya ya
Ludewa.
“Napenda
kuitamburisha kwenu wajumbe wa bodi na wazazi namba ya usajiri ya shule yetu
kwani kwa pamoja tumefanikisha usajiri wa shule yetu kutokana na uvumirivu wenu
wa muda mrefu kama mnakumbuka awali hatukuwa na usajiri lakini tulikuwa na
wanafunzi hivyo kwa yeyote anayehitaji kumleta mtoto wake kuhamia shule ya
msingi nafasi zipo wazi”,alisema Bw.Mwinuka.
Akiwashukuru
wajumbe wa body na wazazi kwa umoja wao mwenyekiti wa body hiyo mzee Ignatio Mirambo alisema kuwa ni muhimu sasa
kuwaelimisha wazazi wa wilaya ya Ludewa na nje ya wilaya ya Ludewa kuitumia
shule hiyo ambayo ni kioo cha jamii ya Ludewa kutokana na mazingira mazuri na
hali ya hewa nzuri ya maeneo ya shule hiyo.
Mzee Mirambo
alisema kuwa baadhi ya wazazi walikata tama kutokana na maneno ya watu kuhusu
kutokuwa na usajiri lakini kwa sasa tayari usajiri umekamilika na tayari shule
ya msingi wanafunzi wamefikia darasa la pili hivyo shule itaendelea kuongeza
majengo na kuboresha mambo mbalimbali ambayo tokea shule hiyo inaanza yamekuwa
ni kivutio cha watu wengi.
Alisema kuwa
tayari shule hiyo imeshasambaza matangazo ya ajira kwa walimu wawili kutoka
nchi za Kenya,Uganda,Zaambia na Malawi ili kuboresha Lugha ya Kingereza kwa
wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo hata hivyo amewataka wazazi kuachana na
tamaduni za zamani za kuwapeleka wanafunzi shule za Serikali hata kama zipo
mbali na maeneo yao wakati shule za watu binafsi ziko mazingira jirani na
mazuri.
mwisho
No comments:
Post a Comment