Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

March 24, 2016

SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA LUDEWA TINSMITH LAWAFUNDA VIJANA

Mwenyekiti wa Ludewa Tinsmisth Bw.Vianely Ngailo

 Katibu wa Ludewa Tinsmith Bw.Bahati Mtweve
 Hivi ni baadhi ya vifaa vinavyotengenezwa na kikundi hicho



Shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe lijulikanalo kwa jina la Ludewa Tinsmith linalojihusisha na utoaji elimu mbalimbali kwa vijana ikiwemo elimu ya ufundi limewataka vijana kujikita zaidi katika kujiajiri kuliko kutegemea ajira kutoka Serikalini ili kujiingizia kipato.


Akitoa taarifa hiyo ofisini kwakwe Mwenyekiti wa shirika hilo Bw.Vianely Ngailo alisema kuwa idadi kubwa ya vijana waliosoma  vyuo vikuu na vyuo vya kati wamekuwa wakishindwa kuendesha maisha yao kwa kusubiri kuajiriwa na Serikali wakati zana hiyo sio sahihi kwani wanapaswa kubuni miradi itakayopelekea kujiajiri na kuwaajiri wengine ili kujipatia kipato


Bw.Ngailo alisema kuwa Ludewa Tinsmith inajishughurisha na mambo mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu ya ufundi kwa fani za,useremala,ushonaji,umakenika na uungaji vyuma ambapo richa ya elimu hiyo ya ufundi pia inatoa elimu ya ujasiliamali kwa watu wanaoishi mazingira magumu ili waweze kujitegemea au kutembea kwa miguu yao wenyewe kiuchumi.


Alisema kuwa shirika hilo lilianzishwa mwaka 1988 lakini limepata usajiri rasmi mwaka 2013 na mpaka sasa limeshafundisha vijana zaidi ya 98 ambao wanawake wanakadiriwa kuwa 38 na wanaume 60  wenye mazingira magumu ambao mpaka sasa wanaendesha maisha yao bila kuwa tegemezi kwa watu wengine au Serikali.


“tungependa vijana wenzetu nchini waige mfano wetu wa kujiajiri wenyewe wanapohitimu elimu ya vyuo kuliko kutegemea serikali kuwaajiri,sisi tunaamini tukijiajiri tunaweza kuzarisha ajira kwa wengine kwakuwafundisha ufundi na kuwaajiri wengine ambao tunaweza kufanya nao kazi kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeisaidia Serikali kwa kiasi Fulani”,alisema Bw.Ngailo.


Bw.Ngailo alisema kuwa shirika hilo linalojiendesha kwa michango ya wanachama richa ya kuwa nitafanya kazi zake bila ya kuwa na ufadhiri wowote nimekuwa likiandika maandiko kuomba vitendea kazi kwa wafadhiri bila mafanikio lakini limekuwa likikabiriwa na changamoto kubwa ya eneo la kufanyia kazi hizo za ufundi kwa limekuwa likipanga katika majengo ya watu hali inayo walazimu wakati mwingine kuingia matatani kutokana na wenye majengo kuwafukuza wakidai huchakaza nyumba zao.


Bw.Ngailo aliiomba Serikali ya wilaya ya Ludewa kutoa Ardhi kwa wadau wa maendeleo kama wao ili waweze kujenga viwanda vidogo vidogo vitakavyowasaidia vijana kujenga ofisi zao ikiwemo na madarasa ya kufundishia kwa vitendo katika viwanda hivyo vidogo.


Aidha mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya alikiri kuchelewa kwa mpango wa utoaji wamaeneo ya viwanda vidogovidogo wilayani hapa hali inayowafanya vijana wengi kushindwa kujiendeleza katika kazi zao za kujitafutia kipato lakini mpango huo upon a utakamilika hivi karibuni ili vijana hao wafanye kazi zao kwa uhuru.


Bw.Choya aliwataka vijana wilayani Ludewa kuiga mfano wa shirika la Ludewa Tinsmith katika kuzalisha ajira kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameongeza ajira kwa vijana wenzao ambao siku zote wamekuwa wakiwa na dhana ya kusubiri kuajiriwa na Serikali.


Mwisho.

No comments: