Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

March 24, 2016

MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA LUDEWA BI. MONICA ACHANGIA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI NA MAZINGIRA HATARISHI LUDEWA MJINI.

Mh.Monica Mchilo akiongea na uongozi wa kituo hicho

watoto wakula chakula cha mchana
Mh.Monica akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chule pamoja na watoto wa mahitaji maalumu



mwandishi wa mtandao huu Nickson Mahundi akiwa na mmoja wa watoto hao




Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ludewa katika mkoa wa Njombe kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Bi.Monica Mchilo ametoa mchango wake wa kilo 20 za sukari katika msimu huu wa sikuu ya Pasaka katika kituo cha watoto wanye ulemavu wa Ngozi na wanaoishi mazingira hatarishi ili kuwaunga mkono kwa jitihada zao za kulea watoto hao.


Akitoa msaada huo Mh.Monic alisema kuwa watoto hao wanahitaji uangalizi mkubwa kwani bado matondo ya kuwakata viungo watu wenye ulemavu wa ngozi hayajafika wilayani Ludewa hivyo ni vema walezi wa watoto hao kuwa makini na baadhi ya watu wanaotembelea kituo hicho ambacho ndio cha kwanza wilayani Ludewa kuanzishwa.


Alisema kuwa msaada huo wa sukari kilo 20 ametoa kutokana na kuguswa na huduma na uendeshaji wa kituo hicho ambacho kinatambulika kwa jina la NICOPOLIS ACADEMY kwani kimekuwa kikiwafundisha watoto hao tofauti na shule nyingine zote za watoto wilayani hapa.


Aliwataka wadau mbalimbali kuchangia kituo hicho ili kuwawezesha watoto hao kupata chakura bora na malazi salama kwani bado kinaendeshwa na wamiliki kwa kujichangisha michango yao hali inayowafanya wamiliki wa chule hiyo licha ya kutoa elimu bora bali kudhohofisha familia zao kiuchumi.


“nimependa uanzishwaji wa kituo hiki kwani nimejionea kwa macho yangu na kusikia kwa masikio yangu elimu wanayopata watoto wadogo kama hawa ambao wanauwezo mkubwa wa kuongea lugha ya kiingereza tofauti na shule nyingine za watoto zilizopo hapa Ludewa Mjini,nawaomba wadau wengine kuunga mkono jitihada hizi ili kuwaendeleza watoto hawa”,Alisema Mh.Monica.


Akishukuru kwa msaada huo mkuu wa kituo hicho Mwalimu Augustino Mwinuka alisema kuwa Diwani huyo ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya  amekuwa mfano wa kuigwa kwa madiwani wengine katika Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwa kushiriki katika mambo ya kijamii.


Bw.Mwinuka alisema kuwa kituo hicho kilianzishwa kwa lengo la kuwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na wale wenye ulemavu wa ngozi kwa kuwapatia elimu bora lakini kutokana na utendaji kazi mzuri wa walimu wa kituo hicho baadhi ya wananchi wameanza kuwaleta watoto wao huku wakichangia kidogo.


Alisema licha ya kuwa kuna baadhi ya hao wazazi walioamua kuwaleta watoto wao na kuchangia gharama nafuu pia kituo hicho kina kabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa majengo na ukosefu wa fedha za kuendeshea kituo hicho.


Bw.Mwinuka alisema kuwa amelazimika kuibomoa nyumba yake aliyokuwa akiishi na kuhama kutafuata nyumba nyingine ya kuishi ili nyumba hiyo itumike kama madarasa ya kusomea watoto hao ambapo amefanikiwa kugawa madarasa mawili ambayo ndio yanayotumika kufundishia.


Alisema kuwa tayari amepata eneo linalokadiriwa kuwa hekali 7 ambazo zinafaa kwa ujenzi wa madarasa,mabweni na viwanja vya michenzo lakini changamoto iliyoko ni ukosefu wa fedha za kufanya ujenzi wa vitu hivyo hivyo anawaomba wadau mbalimbali na wafadhiri kumuunga mkono katika ujenzi wa madarasa hayo kwaajili ya watoto hao wenye mahitaji maalumu.



Mwisho.

No comments: