Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

March 13, 2015

DARASA LA AWALI KATIKA KIJIJI CHA KINGOLE LAEZEKWA KWA NYASI WANAFUNZI WADANDIA MADARASA MENGINE KUHOFIA MVUA

Hili ndilo darasa lililoezekwa kwa nyasi





 Wanafunzi wa darasa la Awali katika shule ya msingi Kingole katika kata ya Masasi wilayani Ludewa wako katika wakati mgumu wa kimasomo kutokana na darasa lao kuezekwa kwa nyasi hali imnayowafanya washindwe kusoma katika msimu huu wa mvua na kudandia vinyumba vya darasa la pili na la kwanza.

Akiongea na mwandishi wa habari hii shuleni hapo mwalimu mkuu wa shule ya Kingole Shamimu Kiyao alisema kutokana na uhaba wa fedha katika Seikali ya kijiji imepelekea darasa hilo kuezekwa kwa nyasi hivyo kushindwa kutumika msimu huu wa mvua kwa wanafunzi hao wa Awali.

Mwalimu Shamimu alisema licha ya kuwa shule hiyo inachangamoto kubwa ya walimu ambapo imekuwa na mwalimu mmoja kwa muda wa mwaka 2014 pia imekuwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa kwa upande wa elimu ya Awali lakini nguvu za wananchi zimeonekana kwa kufyatua tofari na hatimaye kujenga lakini upande wa uezekaji bado ni tatizo.

“Tuanawanafunzi wa awali na tumewatafutia mwalimu wa kujitolea lakini bado changamoto kubwa katika msimu huu wa vyua ni chumba cha kusomea kwani chumba chao kimeezekwa kwa nyasi hivyo kuwafanya kudandia vyumba vya wenzao pale inaponyesha mvua”,alisema mwalimu Shamimu.

Naye ofisa mtendaji wa kijiji cha Kingole Bw.Benedict Ngalawa alisema kuwa darasa hilo la awali ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi limeezekwa kwa nyasi kutokana na kijiji kutokuwa na fedha za kununua bati za kuezekea hivyo kikao cha Serikali ya kijiji kiliazimia wananchi wang’owe nyasi la liezekwe kwanza mambo mengine yatafuata.

Bw.Ngalawa alisema kuwa hata mbao zilizotumika katika kupauwa hilo darasa kuna muhisani alijitolea na kuwalipa mafundi ambaye ni mwananchi wa kijiji cha Kingole aliyemtaja kwa jina la kalumanyile na baadha ya kumaliza kupaua utata ukabaki katika kutafuta fedha za kununua bati.

“Tunamshukuru Kalumanyile kwa kutambua umuhimu wa elimu katika kijiji chake kwani bila kutoa msaada wake jengo hili lingekuwa limeanguka lakini hizi nyasi ziasaidia kuzilinda kuta zisiangunge hivyo bado tunaendelea kutafuta fedha za kumalizia ujenzi ili wanafunzi wa awali wapate sehemu sahihi ya kusomea”,alisema Bw.Ngalawa.

Bw.Ngalawa amewataka wazawa wa kijiji cha Kingole wanaoishi katika miji mbalimbali ndani ya nchi na nje kumuunga mkono Bw.Kalumanyile katika kuchangia maendeleo ya kijiji hicho ambacho kimekuwa na changamoto kubwa ya kielimu hivyo kuwafanya vijana wa hapo kushindwa kupata maendeleo.

Mwisho.

KWA UDHAMINI WA

JANUARY AUTO GARAGE

Wanapatikana Ludewa mjini mtaa wa Kimbila mkabala na sheli ya mafuta katika jengo la John Haule wa Mlangali.

Ni mafundi waliobobea katika utengenezaji wa Magari,Pikipiki na mashine mbalimbali.

Pia wanafanya kazi za welding kuunga kwa kutumia umeme,utengenezaji wa Mageti,misalaba,viti vya Saloon na vifaa vyote vinavyotumia chuma.

Wana parking yakutosha

Kwa mawasiliano wasiliana nao kwa namba 0764962710/0752403545.

KARIBU JANUARY AUTO GARAGE KWA HUDUMA BORA.

No comments: