Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

December 17, 2013

WANAHABARI WILAYANI MAKETE WAASWA KUWA WELEDI

  Waandishi wa habari wameaswa kufuata maadili ya taaluma yao ili kutoviingiza vyombo vya habari katika matatizo na kuipotosha jamii.

Wito huo umetolewa jana na M/kiti wa halmashauri ya wilaya ya makete Mh.Daniel Okoka aliyekuwa mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo ya kuijengea uwezo bodi ya redio kitulo fm pamoja na wakuu wa Idara kwa ufadhili wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini Tanzania Media Fund(TMF) mafunzo hayo yatakayochukua siku 5 kuanzia jana hadi ijumaa ya tarehe 21 disemba mwaka huu

Ktk mafunzo hayo yalihodhuriwa na wanahabari kutoka kitulo fm redio,bodi ya redio na muwezeshaji Dr.Alfred Rwechengula ktk kuhakikisha redio inaingiza kiasi kikubwa cha  mapato kwa njia ya uboreshaji wa vipindi vyenye kuelimisha jamii

Jumla ya wanahabari 10 wameanza kupata mafunzo hayo ili kuelimisha jamii ya wanamakete na nje ya makete pia ili kuongeza uelewa kwa wanajamii hasa katika Nyanja za Elimu,Afya,Mazingira pamoja na Biashara

Redio kitulo fm ambayo ilianzishwa mwaka 2005 kwa msaada wa UNICEF kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Makete 
 
Mh.Okoka ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na wananchi kupata habari za Makete na duniani kwa ujumla kwa wakati muafaka,kuwahamasisha vijana kujishughulisha na maendeleo ktk jamii,imetoa ajira kwa vijana wenye taaluma ya uandishi wa habari na Utangazaji,imesaidia kutangaza matangazo ya halmashauri na kuwafikia walengwa kwa wakati

Hata hivyo amezitaja baadhi ya changamoto ambazo redio inakumbana nazo kuwa ni pamoja na vifaa duni hivyo kutofikia baadhi ya maeneo hata katika wilaya ya makete,kituo kinaingiza mapato kidogo pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wanahabari waliopo kituoni hapa.

No comments: