Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

November 17, 2013

MADIWANI WANGING'OMBE WAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA ZA MAKUSUDI KUKARABATI BARABARA YA USALULE-LUGENGE.




 Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge

Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe

Madiwani Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Wameitaka Serikali Kuchukua Hatua za Haraka Kufanya Ukarabati wa Barabara ya Usalule-Lugenge Yenye Urefu wa Kilomita Nne Ambayo Mvua Zikinyesha Haitoweza Kupitika Tena.

Madiwani Hao Wamesema Endapo Serikali Haitochukua Hatua za Makusudi Katika Kuhakikisha Barabara Hiyo Inajengwa Ili Kuondoa Adha Ya Kukatika Kwa Mawasiliano Kufuatia Kuwepo Kwa Hali ya Kuanza Kwa Mvua Katika Siku za

Usoni.

Agnetha Mpangile ni Diwani wa Kata ya Ulembwe na Esterina Mbwilo ni Diwani Viti Maalumu Tarafa ya Imalinyi Ambao Wamesema Wamekuwa Wakilalamikiwa na Wananchi wa Maeneo Hayo Kwa Kushindwa Kuhamasisha na Kufuatilia Ili Barabara Hiyo Iweze Kulimwa Kitendo Kinachowafanya Kukosa Imani na Wananchi Wao.   

Akijibia Malalamiko Hayo Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Mhandisi Steven Haule Amesema Kuwa Kwa sasa Barabara Hiyo Imekosa Fedha za Dharula Kwa ajili ya Kufanya Ukarabati wa Muda Hivyo Itatengewe Bajeti Katika Awamu Ijayo.

Mhandisi Haule Amesema Barabara Hiyo Ilitumia Kiasi Kidogo Cha Fedha Ambacho ni Zaidi ya Shilingi Milioni 16 Hali Iliyopelekea Barabara Hiyo Kutokuwa Imara.

Kwa Upande Wake Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge Ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Kuomba Fedha za Mfuko wa Dharula Kutoka Kwenye Mfuko wa Taifa wa Barabara Ili Kuwanusuru Wananchi Hao Mara Baada ya Kukatika Kwa Mawasiliano.

No comments: