.
Shirika la
afya dunian (WHO) kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii imeanzisha chanjo mpya kwa watoto wenye umri chini ya
mwaka mmoja itakayoanza January 2013
kutokana na kuona vifo vya watoto wadogo vinazidi kuongezeka .
Hayo
yalisemwa jana na mratibu wa afya mkoa wa Iringa Bi.Mariam Mohamed katika semina ya uchanjaji chanjo kwa watoto
wadogo wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ili kunusuru maisha ya watoto
wadogo ambao kinga yao mwilini haiwezi kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Bi.Mariam
aliitaja chanjo hiyo ni ya kifua kikuu na kuhara kwani ni magonja yaliyofanyiwa
utafiti na kupatiwa ufumbuzi kwa kupitia chanjo kwa watotot wenye umri chini ya
mwaka mmoja.
Alisema
shirika la afya duniani linataka kuhakikisha kuwa kufikia mwaka 2014 chanjo za
Maralia na virus vya Ukimwi ziwe zimepatika na kutokana na magonjwa hayo kuwa
tishio Duniani kwa lika zote.
Bi.Mariam aliwataka wananchi kutambua chanjo
hiyo haitawahusu watoto wenye umri zaid ya mwaka mmoja kwani kinga ya mototo
mchanga ni ndogo ndomana inabidi watoto hao waanze kupatiwa chanjo wakiwa na
wiki sita 6 na akifikia umri wa miezi 9
atapewa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa surua.
Akifungua
semina hiyo mganga mkuu wa wilaya Dr.Happines Ndossi aliyataja baadhi ya magonjwa yatakayotolewa chanjo kuanzia January 2013 kwa watoto hao ni pamoja
na kifua kikuu, surua, kupooza, pepopunda, dondakoo, kuhara na nimonia.
Dr. Ndossi aliwataka wazazi wenye watoto
wadogo kuhamasika kutokana na chanjo hiyo hasa kwa wale wanaotokea mbali na
vituo vya afya kwa lengo la kuboresha afya ya mtoto pasipo kutupilia mbali
suala la usafi wa mazingira, kuwepo kwa vyoo bora na chakula safi.
Kwaupande
wake mganga mkuu wa wilaya Dr. Ndoss alizitaja changamoto zitakazowakumba
kutokana na chanjo itakayoanza January 2013 ni pamoja na baadhi ya wananchi na viongozi wa dini
kutokuwa na uelewa juu ya chanjo hiyo pamoja na kukosa wasaidiz ambalo tatizo
hilo lipo juu ya uwezo wao vituo vya afya wilayani humo kuwa vingi.
“wasaidizi
wanahitajika 30 lakini waliopo hadi sasa hawazidi 8 na maafisa wakuu wapo 4 ni
zoezi ambalo ni changamoto kubwa kwa idara ya afya kuweza kuweza kufanikisha
zoezi zima la uchanjaji chanjo kwa watoto wadogo”alisema Dr. Ndossi.
Dr. Ndoss
alionyesha mfano wa vichupa vya dawa ambavyo vinatumika kuhifadhia dawa ya
chanjo ya kuhara ambayo inagharimu dola 35 yenye thamani y ash. 5600 kwa kila
kityubu na wizara ya afya na ustawi wa jamii inahusika kupanga bajeti ya chanjo
hiyo.
Naye mh.
Diwani wa kata ya Ludewa bi. Monika Mchilo akizungumza katika semina alitilia
mkazo zoezi la usafi kwa kuwataka viongozi wa afya wa wilaya ya ludewa
kusimamia ipasavyo kabla zoezi la chanjo kwa watoto hao halijaanza kwani
itasababisha magonjwa mengi ikiwemo kipindupindu.
Zoezi hili
la chanjo kwa watoto wadogo ni zoezi la kitaifa na kila mwananchi anahitajika
kuwajibika kwani semina hii imefanyika katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya
kata mkoa hadi kata.
MWISHO
No comments:
Post a Comment