wananchi wa kijiji cha Amani wakicheza ngoma ya Asili ya kipangwa na picha ya chini Mh.Mgina akitoa maelezo kwa viongozi mbalimbali kuhusiana na ujenzi wa mabweni hayo
Ujenzi wa majengo mengine katika shule hisho unaofadhiriwa nashirika la shipo ukiwa unaendelea katika shule ya sekondari Mundindi
mh.Mgina na raia wa kihoranzi kutoka shirika la shipo wakiuonesha uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa majengo hayo majengo ya mabweni ya wasichana katika shule ya sekondari ya Mundindi yaliyojengwa na Uhoranzi
UMOJA wa wanafunzi wa Uholanzi chini ya Shirika lisilo la
kiserikali la Shipo linalojishughurisha na kutoa huduma kwa jamii mkoani Njombe
limekabidhi mabweni mawili ya wasichana yenye
thamani shilingi 60 milioni kwa ajili ya
Shule ya Sekondari ya Mundindi
wilayani Ludewa.
Mabweni hayo
yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wa
kike zaidi ya sabini yamejengwa kwa ushirikiano kati ya mfadhiri huyo na
wananchi wa kata ya Mundindi, umoja wa wanafunzi wa uholanzi umekuja baada ya
kukithiri kwa mimba na utoro kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya mundindi
kunakotokana na wachimbaji madini.
Akikabidhi
mabweni hayo Afisa ufundi wa shirika la SHIPO ambaye pia ni Diwani wa kata ya
Mundindi Mh.Vincent Mgina alisema ujenzi wa shule hiyo ulianza rasmi mwaka 2011
ambapo wanafunzi wa Uhoranzi kupitia SHIPO alianza kuifadhiri shule hiyo.
Mh.Mgina
alisema kutokana na uhusiano mzuri ulijengwa na wanafunzi wa Uhoranzi na
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mundindi uliiwezesha shule hiyo kujengwa
haraka na kwa majengo mazuri tofauti na shule nyingine wilayani Ludewa.
Alisema
ujenzi huo SHIPO walifadhiri viaa vya viwandani na mbao wakati wananchi wa kata
ya mundindi walijitolea nguvu zao ikiwemo ufyatuaji wa tofali na ujenzi hali
ambayo iliwatia moyo wafadhi ambao wamepanga kuendelea kuifadhiri shule hiyo.
“shirika
letu limeona ushiriki wa wananchi wa Mundindi katika maendeleo yao kutokana na
wanavyojitoa kufanya kazi za ujenzi wa shule hii hivyo wafadhiri wanataka kuona
shule hii inaendelea kuwa bora zaidi ya shule nyingine katika wilaya ya
Ludewa”,alisema Mh.Mgina.
Mh.Mgina
alisema licha ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni hayo shirika lake
limetengeneza vitanda 35 vyenye uwezo wa kulaza wanafunzi 70 lakini limeahidi
kujenga mabweni manne na ukumbi wa kujisomea utakaokuwa na uwezo wa kuchukua
wanafunzi 274 .
Hata hivyo
ujenzi wa nyumba ya matroni na mabweni ya wanafunzi wa kike unaendelea ili
kupunguza uwezekano wa wanafunzi wa kike kupata ujauzito ambao utawakatishia
masomo yao.
Aidha Mgeni
rasmi katika makabidhiano Mh.Mathei Kongo ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri
ya wilaya ya Ludewa na Diwani kata ya Luilo alisisitiza wanafunzi na wananchi
wa Mundindi kuitunza shule hiyo na vifaa vilivyomo kwa kuzingatia shule hiyo
imejengwa kisasa zaidi.
Mh.Kongo
aliliomba shirika hilo kutengeneza uzio wa kuizunguka shule hiyo kutokana kuwa karibu na maeneo ya machimbo ya chuma
cha liganga na mashimbo ya dhahabu kjiji cha Amani ambako shule hiyo imejengwa.
Alisema uhusiano
mzuri walioujenga wanafunzi wa shule ya sekondari Mundindi na wanafunzi wa
Uhoranzi kupitia shirika la SHIPO unafaa kudumishwa ili kuleta changamoto ya
maendeleo katika kata nyingine zisizo na wafadhiri ambapo wataweza kuiga
utendaji kazi wa wananchi wa Mundindi.
Mh.Kongo aliishukuru
Uhoranzi kupitia shirika la SHIPO kwa kutoa hundi ya shilingi za kitanzania 70
milioni katika hafla hiyo ili kuendeleza ujenzi wa nyumba ya matroni na mabweni
ya wasichana yanayoendelea katika ujenzi.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment