MAHAKAMA ya hakimu
mkazi Wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe mbele ya hakimu Fredrick Lukuna imemtia
hatiani na kumhukumu kijana mmoja kuchapwa viboko 12 kwa kumbaka mtoto wa kike
mwenye umri wa miaka 11 na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Awali ilidaiwa
mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa polisi mkaguzi wa polisi Peter Majengo
kuwa mshtakiwa Richard Msemwa 17 mkazi wa kijiji cha Luafyo juu katika kata ya
Lugarawa alitenda kosa hilo juni 13 mwaka huu.
Majengo akaiambia
mahakama ya hakimu mkazi kuwa mshtakiwa Richard Msemwa siku ya tukio aliwafuata
watoto hao mtoni walipokwenda kuchota maji naye kuwavizia na kumkamata mtoto
Jenifer Mwinuka na kumbaka vibaya.
Akisoma hukumu hiyo
iliyochukua masaa takribani mawili hakimu mkazi Fredrick Lukuna wa mahakama ya
wilaya ya Ludewa akasema mahakama yake imeridhika na ushahidi uliotolewa na
upande wa mashtaka na kwamba hakuna shaka lolote kwamba mshtakiwa hakutenda
kosa hilo.
Akasema ushahidi wa
ripoti ya daktari pamoja na vielelezo vyote vilivyotolewa mahakamani hapo
ndivyo vilimtia hatiani mshtakiwa huyo.
Akitoa amri Lukuna
akasema kutokana na mshtakiwa kuwa na umri mdogo wa chini ya miaka kumi na saba
mahakama inamtia hatiani na kwamba mshtakiwa anahukumiwa kuchapwa fimbo kumi na
mbili matakoni lakini baada ya daktari kuthibitisha afya yake.
Akitoa maombolezo na
utetezi kwa hakimu ili asipewe adhabu kali mshtakiwa Richard Msemwa aliomba
apunguziwe adhabu kwa kuwa hakutenda kosa hilo Lakini mwendesha mashtaka
akaitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kwa kuzingatia uzito wa kosa
ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo ili kupunguza makosa
kama hayo katika jamii, ingawa mwendesha mashtaka aliiambia mahakama kuwa ofisi
yake haina kumbukumbu ya makosa ya nyuma kuhusu mshakiwa huyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment