Wakulima wakimsikiliza mkuu wa wilaya wakati akimfukuza mlinzi wa NFRA
Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Ludewa Bw.Edings Mwakambonja akiongea na wakulima
Baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ludewa akimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ludewa
Mwakambonja akisisitiza jambo
wananchi wakiwa mkutanoni
Mkuu wa wilaya ya Ludewa
Bw.Juma Solomon Madaha amemfukuza mlinzi wa wakala wa uhifadhi wa chakula
nchini(NFRA)katika kituo cha manunuzi ya mahindi kilichopo Ludewa mjini
kutoonekana tena wilayani hapa na kurudi kwao Mkambako kutokana na kutuhumiwa
na wakulima kuwa amekuwa akifanya vitendo vya rushwa na kusababisha wakulima
wadogo kushindwa kuuza mahindi yao.
Bw.Madaha alitoa amri ya
kuondolewa haraka mlinzi huyo jana aliyetambulika kwa jina la Linus Mwifunye na
Jeshi la Polisi wilayani Ludewa na kumrejesha katika ofisi kuu ya NFRA
Makambako ili kulinda usalama wake kutokana na minong’ono ya wananchi kutaka
kumdhuru mlinzi huyo kwa vitendo vyake vya kupitisha maloli ya mahindi ya
wafanya biashara badala ya wakulima wadogo..
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara na wakulima jana katika kituo cha Ludewa mjini ambako mpango wa
Serikali wa kununua mahindi kwa wakulima unaendelea Bw.Madaha alisema amefikia
uamuzi wa kumfukuza mlinzi huyo katika mji wa Ludewa kutokana na malalamiko
mengi aliyoyapokea kutoka kwa wakulia hali ambayo ilikuwa inatishia usalama wa
mlinzi huyo.
Alisema licha ya kuwa Serikali
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka kununua mahindi kwa wakulima wadogo
nchini lakini baadhi ya wafanyakazi wa NFRA wamekuwa si waaminifu kwani
wamekuwa wakitumiwa na walanguzi na kuyapitisha mahindi ya walanguzi hao ili yaweze
kuuzika na kuwaacha wakulima ambao ndio waliolengwa na mpango huo.
“alipita mkuu wa mkoa hapa na
akatoa maagizo kuwa wakulima wadogo ndio wanaotakiwa kuuza mahindi yao lakini
imekuwa sivyo, kwani mahindi yaliyoko hapa yalitakiwa yawe yameshapimwa nashangaa mpaka sasa bado na kila siku
upimaji unaendelea na wananchi wangu wanapingwa na jua hapa kila siku bila
mafanikio kutokana na mlinzi kuingiza mahindi usiku ya wafanyabiashara hivyo
kwa mamlaka niliyonayo naamuru aondoke haraka katika wilaya yangu kwa
kusindikizwa na Polisi”,Alisema Bw.Madaha.
Bw.Madaha alisema hata mfumbia
macho mtu yeyote atakayetaka kuwaumiza wananchi wake katika haki yao hivyo
aliwataka wafanyakazi wa NFRA kufanya kazi waliyotumwa ya kununua mahindi kwa
wakulima wa hali ya chini kwaajili hifadhi ya Taifa na si kuungana walanguzi
katika kuwanyonya wakuliwa hao wa hali ya chini kwani ameshapata taarifa hizo
za vitendo ya unyonyaji katika vituo vyote vya ununu wilayani Ludewa
vinavyofanywa na maafisa wa NFRA kwa kushirikiana na walanguzi.
Naye Diwani wa kata ya Ludewa
Mjini Mh.Monica Mchilo alisema malalamiko hayo ni ya muda mrefu kwani mlinzi
huyo aligeuka kuwa Mungu mtu kutokana na tabia yake ya kuwahada wakulima kwa kuwaeleza watoe
hela ili waweze kupata namba ya kupima mahindi haraka bila kufanya hivyo
ataendelea kuingiza mahindi ya walanguzi hali ambayo wakulima hao waliona kuwa
wametelekezwa na Serikali yao.
Mh.Monica kutokana na mahindi
kuwa mengi katika kituo hicho uongozi wa kijiji uliweka bango ambalo
lilisitisha wakulima wengine kuleta mahindi katika kituo hicho mpaka yaliyopo
yamalizike kupimwa ili kutoa nafasi ya NFRA kupanga magunia yao lakini
chakushangaza mlinzi huyo na baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu walikaidi
agizo hilo na kupitisha maloli ya mahindi nyakati za usiku.
Katibu wa umoja wa wakulima na
wauzaji wa mahindi katika kituo hicho Bw.Aurelian Mhagama (AMCA) alisema bila
kufika uongozi wa Serikali ya wilaya ya Ludewa kituoni hapo hali ingekuwa mbaya
zaidi kutokana na mlinzi huo na baadhi ya uongozi wa kijiji kuliteka soko hilo
la mahindi kwa kuwanyonya wakulima wadogo kwani jitiada zake na viongozi wenzie ndizo zilifanya
viongozi hao wafike ili kujionea hali halisi.
Bw.Mhagama alisema licha ya
kuwa mlinzi huyo kuwahujumu wakulima pia hata makuli wamekuwa tatizo kubwa
kwani wamepatisha bei ya ubebaji maroba ya mahindi kutoka shilingi 1000 hadi
shilingi 3500 kwa roba moja lenye madebe nane kutoka umbali wa mita tano hadi
kwenye mzani,hali hiyo inawaumiza sana wakulima na kukatishwa tamaa ya
kuendelea na kilimo cha mahindi msimu ujao.
Alisema wakulima wengi wa hali
ya chini wahana fedha kwa sasa za kumudu kulipia ubebaji huo lakini wamekuwa
wakilazimishwa kulipia ubebaji kabla ya kazi kuanza na hata kama unavijana wako
nyumbani wa kubeba mahindi yako ukitaka kufanya hivyo makuli hao kutoka
Makambako wamekuwa wakizuia kwa kisingizio cha kuwa wao ndio wanaelewa namna ya
uwekaji mahindi hayo katika mzani hali ambayo si kweli.
Bw.Mhagama aliitaka Serikali
kuliangalia hilo pia kwani mpaka sasa hakuna faida yoyote anayoweza kuipata
mkulima wa kawaida kwa kuuza mahindi yake zaidi ya unyanyasaji unaoendelea
katika vitu vyote vya wilaya ya Ludewa toafauti na matarajio ya wakulima hao
awali walipoelezwa na viongozi wa Serikali.
Aidha kamanda wa taasisi ya
kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Ludewa Bw.Edings Mwakamboja
aliwataka wakulima hao katika vituo vyote wilayani huo kutoa ushirikiano kwa
kutoa taarifa pale wanapoona kuna dalili ya vitendo vya rushwa kwani hakuna
hata kituo kimoja ambacho hakina malalamiko hayo lakini ofisi yake inapojaribu
kufuatilia hakuna ushirikiano kutoka kwa wakulima wenyewe.
Bw.Mwakambonja alisema ni
kweli walanguzi wamekuwa wakilalamikiwa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa NFRA
lakini hakuna mkulima anayeweza kujitokeza hadharani akisema ameombwa
rushwa hivyo hakuna haja ya kuficha
jambo kama wakulima hao watataka kutendewa haki katika kuuza mazao yao kwa
kuhakikisha suala hilo linakomeshwa alitoa
namba yake ya simu ya mkononi kwa wananchi wote ili kumjulisha pale wanapoona
kunadalili ya rushwa kwa kufanya hivyo ofisi yake itaweza kutega mtego wa
kuwanasa wanaojihusisha na rushwa hizo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment