Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

August 27, 2013

UTATA WA MASHAMBA KWA WAKULIMA WANGAMA WILAYANI WANGING'OMBE WASULUHISHWA.



Maeneo ya Kujenga Makao Makuu wanging'ombe yaanza Kupimwa.

Zoezi la Ugawaji Mashamba ya Wakulima waliokubali Kupisha Eneo la Kujenga Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe Limetajwa Kuendelea Vizuri kwa Wananchi wa Igwachanya baada ya Zoezi Hilo Kukamilika Kwa wananchi wa Kijiji cha Chalowe.

Akizungumza na mtandao huu Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Igwachanya Bwana Petro Ndone Amesema Kuwa Jumla ya Ekari 12 zinaendelea Kutolewa katika Maeneo Mbalimbali ya Vitongoji vya Kijiji cha Igwachanya  kwa wananchi sita Ambao ni Miongoni mwa Wakulima waliokuwa wakilima Katika Eneo la Ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe.

Mwenyikiti Ndone Amesema Kuwa Wananchi watatu walipewa Mashamba hayo Jana Katika Kitongoji cha Makungu na Leo zoezi hilo linaendelea Kukamilishwa kwa Wananchi watatu Waliosalia Katika

Kitongoji cha Igombatavangu .
Katika Hatua Nyingine Amesema Kuwa Kukamilika kwa Zoezi hilo bila Tatizo kutapelekea zoezi la Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya Hiyo Kwenda Vizuri kwani Hadi sasa Upimaji wa Maeneo unaendelea Vizuri.

Yob Sahara ni Miongoni mwa wananchi wanaoendelea Kupatiwa Maeneo hayo ambaye Amepongeza hatua ya Serikali Kuwagawia Mashamba hayo hata Kama yanapatika mbali na Maeneo waliyokuwa wakiyalima.

Hata Hivyo Wananchi Hao wamesema kuwa Kitendo cha Serikali Kukubali Kuwaonesha Maeneo Mengine Kumewafanya kuacha Malalamiko waliyokuwa nayo hapo Awali hali iliyopelekea Kuyafikisha kwa Mbunge wao.

 Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe

No comments: