Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

July 11, 2017

LUDEWA RANGERS FC YAIBUKA MSHINDI KATIKA MASHINDANO YA SIKUKUU ZA SABASABA WILAYANI LUDEWA.

Wachezaji wa timu ya Ludewa Rangers wakiwa na furaha baada ya kuichapa timu ya vijana stars goli mbili kwa moja na kuwa washindi wa mashindano ya sikukuu ya sabasaba wilayani Ludewa mwaka 2017
Wachezaji wa timu ya Ludewa Rangers wakiwa na furaha baada ya kuichapa timu ya vijana stars goli mbili kwa moja na kuwa washindi wa mashindano ya sikukuu ya sabasaba wilayani Ludewa mwaka 2017 
 Mratibu wa Ludewa Education Centre Mwalimu Augustino mwinuka akitoa ripoti ya kituo hicho baada ya pambano kuisha


  Mratibu wa Ludewa Education Centre Mwalimu Augustino mwinuka akitoa ripoti ya kituo hicho baada ya pambano kuisha
 Vijana wa Ludewa Rangers wakisalimiana na viongozi baada ya kupokea zawadi yao
 wachezaji wa vijana stares wakisalimiana na viongozi baada ya kupokea zawadi ya mshindi wapili


 Charles Keiya akiongea na mashabiki wa soka baada ya mashindano kumalizika

Viongozi mbalimbali wakifuatilia pambano
 Katibu wa mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Fungatwende akiongea na mashabiki wa soka baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi.



Ludewa Rangers Fc imeibuka kidedea katika mashindano ya mpira wa miguu  ya sherehe za sabasaba wilayani Ludewa kwa kuifunga timu ya Vijana stars kwa goli nne kwa moja mashindano hayo ambayo yaliandaliwa  na Ludewa Education Centre yaliyofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu Ludewa mjini.

Akisoma risala baada ya kuhitimisha mashindano hayo Mratibu wa Ludewa Education Centre Mwalimu Augustino Mwinuka alisema kuwa kituo hicho ambacho madarasa yake yako katika majengo ya CCM kilianzishwa  na mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Endrea Tsere akiwa na lengo la kukuza elimu wilayani Ludewa.

Mwalimu Mwinuka alisema kuwa mpaka sasa kituo hicho kinawanafunzi wengi wengi wao wakiwa ni vijana hivyo ni fulsa pekee hata wachezaji wa mpira wa miguu ambao hawakuipata elimu kujiendeleza ili kupata elimu ya Sekondari ambayo itawasaidia kupanua uelewa na kuwasiliana na wachezaji wa timu za mataifa mengine kwa Lugha ya Kingereza.

Akitoa zawati wa washindi wa mashindano hayo ya sabasaba wilaya ya Ludewa kwa mwaka 2017 katibu wa mbunge wa jimbo la Ludewa kwa niaba ya mbunge wa jimbo la Ludewa ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi wa kufunga mashindano hayo katibu wa mbunge Bw.Fortunatus Fungatwende alisema kuwa wakati umefika sasa wanamichezo kutambua umuhimu wa elimu kwani ndio msingi wa maisha.

Bw.Fungatwende alisema kuwa Ludewa Education Centre inamalengo makubwa katika elimu ya wilaya ya Ludewa hivyo vijana wanapaswa kuchangamkia fulsa hiyo ili kutimiza malengo yao aidha aliwapongeza Ludewa Rangers fc kwa kuibuka washindi wa mashindano hayo kwani ni vijana wenye umri mdogo hivyo wanaweza kusonga mbele zaidi kama wataamua kujiwekea malengo.

Naye afisa tawala wa wilaya ya Ludewa Bw.Charles Keiya kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ludewa aliwataka wanamichezo kukitumia kituo hicho kama sehemu muhimu ya kujipatia elimu kwa muda mfupi ili kwenda na soko la ajira hasa ya kimichezo Duniani.

Mwisho.

No comments: