Baadhi ya majengo ya shule ya Morning Star Ludewa
Uongozi wa shule ya Morning star ukiwa katika kikao pamoja na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo.
Baadhi ya majengo ya shule ya Morning Star Ludewa
Wazazi wakiwa katika kikao shuleni Morning Star wakijadili namna elimu gani ya uboreshwaji wa elimu katika shule hiyo.
Wazazi wakiwa katika kikao shuleni Morning Star wakijadili namna elimu gani ya uboreshwaji wa elimu katika shule hiyo.
Shule ya
msingi ya Morning star iliyosajiliwa kwa
namba IR.05/3/002 ndani ya shule hiyo
kuna shule ya awali ilyosajiliwa kwa namba IR.05/3/EA.002 inayopatikana
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ilianza
mwaka 2014 ikiwa na wanafunzi wachache mwanzilishi na mmiliki wa shule
hiyo akiwa Bw.Maulid Mwingira.
Bw.Mwingira
aliianzisha shule hiyo kutokana na ukweli kwamba kulikuwa hakuna shule binafsi
ya watoto wadogo ndani ya wilaya ya Ludewa hivyo iliwalazimu baadhi ya wazazi
wenye uwezo mzuri wa kifedha kuwapeleka watoto wao katika shule binafsi za
wilaya ya Njombe na mkoa jirani wa Mbeya.
Baada ya
uanzishwaji wa shule hiyo iliwasaidia wazazi hao kupunguza gharama kwa
kuwarudisha watoto wao kutoka wilaya na mikoa mingine na kubaki shule ya
Morning star ambako walianza kutoa elimu ambayo ilikuwa ikitafutwa katika
wilaya na mikoa mingine ikiwa ni kufundihswa kwa Lugha ya Kingereza kwa watoto
wadogo.
Shule hiyo
ambayo kwa hivi sasa inasimamiwa na kaimu Mkurugenzi ambaye ni Bw.Augustino
Mwinuka awali alikuwa mwalimu mkuu wa
shule hiyo na baada ya kuendelea kuwazoesha wakazi wa wilaya ya Ludewa kutumia
shule binafsi tofauti na walivyozoea awali kwa kuzitumia shule za Serikali
tu,imekuwa na mafanikio makubwa ya kuwa na wanafunzi wengi wanaohamia na
kujiunga na masomo katika shule hiyo.
Bw.Mwinuka
anasema kuwa uanzishwaji wa shule hiyo umeleta mabadiriko makubwa katika sekta
ya elimu wilayani Ludewa kwani wazazi wamekuwa na uchaguzi wapi watoto wao
wanaweza kupata elimu kwani awali wengi hwakuona umuhimu wa uanzishwaji wa
shule hiyo ya Morning Star.
“Tumeanza
kuona wazazi wanawaleta watoto wao hapa tofauti na awali hivyo kwa sasa usajiri
umekamilika na hata wanaohamia ni wengi
kwani wameona ubora wa elimu tunayoitoa hapa imeonekana ni bora kuliko maeneo
mengine hivyo ndio sababu ya wazazi wengi kuwahamisha watoto wao maeneo mengine
na kuwaleta katika shule hii”,alisema Bw.Mwinuka.
Hata hivyo
Bw.Mwinuka aliwataka wazazi kutoa ushirikiano katika mambo mbalimbali
yanayoihusu shule hiyo ili kufanikisha malengo ya elimu bora kwa wanafunzi
wanaosoma Morning Star.
Mwisho.
TANGAZO
MTANZANIA RESTAURANT LUDEWA.
MTANZANIA RESTAURANT, WANAPATIKANA LUDEWA MJINI KATIKA JENGO LA NDICHELIWE.
KWA CHAKULA SAFI NA BORA UKIFIKA LUDEWA MJINI MTANZANIA RESTAURANT NDIO SURUHISHO PIA KWA CHAKULA CHA MAHARUSI,MISIBA MAHAFARI NA SHEREHE MBALIMBALI
KWA MAWASILIANO PIGA NO.0758146258 au 0624985168 KWA CHAKULA CHA UHAKIKA.
No comments:
Post a Comment