Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Edward Haule akionesha eneo la uchimbaji wa barabara hiyo kushoto kwake ni Diwani wa kata ya milo Mh.Elisha Haule
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Edward Haule na Diwani wa kata ya Milo Mh.Elisha Haule pamoja na Raia wa Marekani wakichimba barabra
Diwani wa kata ya Mkongobaki Mh.Mtweve akiwajibika katika maendeleo ya uchimbaji wa barabra hiyo.
Diwani wa kata ya Mkongobaki Mh.Mtweve akiwajibika katika maendeleo ya uchimbaji wa barabra hiyo.
Wananchi wakichimba barabra hiyo
Mwandishi wa Mtandao huu Nickson Mahundi akisaidiana na wananchi katika uchimbaji wa barabara
Mh.Edward Haule akiendelea kutoa maelekezo
Wanahabari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushirikiana na wanachi wa kijiji cha Milo na Lipangala wilayani Ludewa katika kuchimba barabra
Gari ya Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ikipita katika barabara mpya inayounganisha kijiji cha Milo na Lipangala bara baada ya kuchimbwa na wananchi.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa na Diwani wa kata ya Ibumi wilayani Ludewa
katika moa wa Njombe ameendelea kuwa mfano wa kuigwa miongoni mwa jamii
kutokana na uwezo wake wa kuwashawishi wananchi katika uanzishwaji wa barabara
za vijijini.
Hali hiyo imedhihirika
jana katika kijiji cha milo na kijiji cha lipangala wilayani hapa ambapo
Mh.Haule kwa kushirikiana na wananchi wa vijiji hivyo viwili waliweza kufanya
harambee ya uanzishwaji wa barabara yenye urefu wa kilometa saba ambayo imekuwa
ni kukwazo katika maendeleo na mawasiliano ya vijiji hivyo.
Akiongea
mara baada ya kukamilisha uchimbaji wa barabara hiyo mh. Haule alisema kuwa
amekuwa na uzoefu mkubwa katika kazi hiyo richa ya kuwa hajasomea uhandisi wa
barabara lakini mpaka sasa ni vijiji vingi vya wilaya ya Ludewa ameifanya kazi
hiyo ikiwa na vijiji vya kata ya Ibumi ambako ndiko alichaguliwa kuwa Diwani.
Mh.Haule
aliwasifu viongozi na wananchi wa vijiji
vya Milo na Lipangala kwa kujitokeza kwa wingi na kuunga mkono juhudi zake za
kuviunganisha vijiji vya wilaya ya Ludewa vilivyopo jirani katika miundombinu
ya barabara kwani maeneo mengine watu hawana imani kuwa bado kunawananchi wenye
uwezo wa kujiletea maendeleo yao wenyewe bila kuisubiri Serikali.
Alisema kuwa
awali alipowasirisha wazo hiyo akiwa na madiwani wa kata ya Milo na Mkongobaki katika
mkutano wa hadhara baadhi ya wananchi walibeza juhudi hizo bila kujali umuhimu
wa barabara hiyo lakini baada ya kukubariana na kuingia kazini bila kujari
itikadi za vyama vya siasa kila mmoja ameona kuwa ukweli wa neon umoja ni nguvu
na utengano ni dhaifu.
“kila mmoja
hakuamini wakati natoa wazo hili la kuichimba barabara kwa mikono yetu wenyewe
ni niliwaeleza kuwa mimi ni mzoefu wa kazi hizi lakini leo mmeamini na mmeona
gari nililokuja nalo limepita vizuri hivyo naomba kwa umoja huu mliouonesha leo
muendelee nao katika mambo mengine bila kujali itikadi zenu za vyama ili
kujiletea maendeleo kuliko kuisubiri Serikali kwa kila jambo”,alisema Mh.Haule.
Diwani wa
kata ya Milo Mh.Elisha Haule akiwapokeza
wananchi wa kata yake katika kijiji cha milo kwa kuitikia wito wa kuchimba
barabara ya kuunganisha kata yake na kata ya Mkongobaki kupitia kijiji cha
Lipangala alisema kuwa Mh.Edward Haule ni mfano wa kuigwa katika madiwani wa
Halmashauri ya wilaya ya Ludewa,kwani anajitoa kufanya kazi bila ya kujali kata
hiyo yuko nani.
Mh.Elisha
alisema kuwa barabara hiyo inaumuhimu mkubwa kati ya vijiji hivyo viwili kwani
wananchi wa kijiji cha Lipangala awali iliwalazimu kutembea umbali mrefu hadi
Lugarawa kufuata huduma za hospitari lakini kwa uanzishwaji wa barabara hiyo
watatumia muda mfupi kutibiwa Milo badala ya Lugarawa.
Aliwataka
wananchi kuitunza barabara hiyo ili iendeleze mahusiano mazuri baina ya vijiji
hivyo kwani wananchi wake ni ndugu lakini kutokuwa na barabara ilikuwa ni
kikwazo kikubwa kutembeleana hivyo ni fulsa nyingine hata kibiashara baina ya
wananchi hao.
Aidha Diwani
wa kata ya Mkongobaki Mh.Ally Mtweve aliyasifu mashirikiano hayo ambayo dhahiri
yameonesha mwelekeo wa kimaendeleo kwani kwakufanya maendeleo wananchi wameweza
kubadirishana mawazo na kupeana fulsa zinazopatikana katika kijiji kingine.
Mh.Mtweve
aliwaomba viongozi wa vijiji kuwachukulia hatua kali kwa wale wananchi
waliofika kuchimba barabara hiyo kwani kwakutofika kwao kunawakatisha tama wananchi
wenye nia njema ambao walijitokeza na kukamirisha kazi hiyo pia aliwapongeza
baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo ambao wanaoishi nje ya wilaya ya Ludewa kwa
kujitolea kununua vitendea kazi ambavyo viliwapa hamasa zaidi wananchi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment