Daraja la mto ketawaka Linalounganisha kijiji cha Maholong'wa na kijiji cha Amani
Bw.Tom Kijumbe kutoka EKA campany Ltd ndiye msimamizi wa ujenzi wa daraja la mto Ketawaka
Mh.Frank Mseya Diwani wa kata ya Ludende
Barabara ya kijiji cha Aman kata ya Mundindi inayoelekea kijiji cha Maholong'wa kata ya Ludende
Daraja la mto ketawaka Linalounganisha kijiji cha Maholong'wa na kijiji cha Amani
Daraja la mto ketawaka Linalounganisha kijiji cha Maholong'wa na kijiji cha Amani
Bw.Kijumbe na Mh.Mseya wakiwa na Furaha baada ya kumaliza ujenzi wa daraja hilo
Ujenzi wa
daraja la mto Ketawaka linalounganisha vijiji vya Amani na Maholong’wa wilayani
Ludewa katika mkoa wa Njombe umekamilika rasmi ambao ni kiunganishi kikubwa
kati ya vijiji hivyo viwili kwani kabla ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo
wananchi walilazimika kutumia njia ya umbali mrefu ambayo ilikuwa ikiwagharimu
fedha nyingi.
Daraja hilo
ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu ambapo ukosefu wa daraja hilo
ulisababisha mara kadhaa vifo kwa wananchi kufa maji pale walipojaribu
kutengeneza madaraja ya mianzi ili kuweza kujinasibu na uvukaji ili kufanya
shughuri za kibinadamu limekamilika kipindi ambacho ni msaada mkubwa kwa
wakulima hasa msimu huu wa mavuno.
Akiongea na
mwandishi wa habari hii msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo Bw.Tom Kijumbe kutoka
kampuni ya EKA ya Jijini Dar es Salaam alisema kuwa richa ya kuwa daraja hilo
limechukua muda mrefu lakini ni daraja bora zaidi kutokana na ukubwa wa mto
Ketawaka,kwani awali wananchi walikuwa na malalamiko mengi wakitaka liishe kwa
haraka lakini hivi sasa wameamini nini EKA Campany Ltd walikuwa wakifanya
katika ujenzi huo.
Bw.Kijumbe
alisema kuwa EKA Company Ltd ni kampuni yenye uzoefu katika kazi hizo za ujenzi
wa madaraja,barabara na majengo kwa muda wa mika 24 hadi hivi sasa hivyo
wananchi hawakutakiwa kuwa na haraka kiasi hicho na walichokuwa wanatakiwa
kusubiri wataalamu wafanye kazi yao ambayo hivi sasa kwa macho inaonekana
tofauti na matarajio ya wananchi wenyewe.
“Tumekuwa na
uzoefu mkubwa katika kazi hizi na daraja hili sio la kwanza na kumekuwa na
maneno ya kuwadharau wakandarasi wazawa na kuwathamini wan je hali ambayo siyo
sawa kwani wahandisi wetu wanasoma vyuo ambavyo vinatambulika kimataifa hivyo
hata hapa kuna baadhi ya watu walibeza lakini sasa kila mmoja anakuja kuangalia
na kusifu kazi iliyofanyika na mtanzania Mwenzao”,alisema Bw.Kijumbe.
Aidha Diwani
wa kata ya Ludende Mh.Frank Mseya alisema kuwa daraja hilo ni ukombozi mkubwa
kwa wananchi wa kata ya Ludende na Mundindi kwani ni barabara fupi zaidi ya
kuja makao makuu ya wilaya ukiachana na umuhimu wake kwa wakulima na wafanaya
biashara.
Mh.Mseya
ameipokeza Serikali kwa kuwakumbuka wananchi wa maeneo hayo kwa kuwajengea
daraja la kisasa ambalo litainua na kukuza kipato kwa wananchi wa maeneo hayo
pia aliwataka wananchi kulilinda ili kuepusha watu wenye nia mbaya ambao huiba
vyuma vya pembeni ambavyo vimechomelewa ili kuzuia watu au vyombo vya moto
kutumbukia mtoni.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment