Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

March 19, 2016

VIJANA WA WILAYA LUDEWA WAMUUNGA MKONO RAIS JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUANZISHA VIKUNDI NA KUACHA KUCHEZA POOL,

Samaki waliovuliwa katika mabwaya ya vijana hao wakiwa tayari kwa kuuzwa
vijana wa Ludewa Ash-tech group wakiendeleza uchimbaji wa mabwawa mengine ya samaki

hili ni moja ya mabwawa ya Samaki ambalo bado linavifaranga
Hili ni moja ya Bwawa ambalo tayari Samaki wake wako tayari kuvuliwa

 Vijana wa Ludewa Ash-tech group wakiwavua samaki katika mabawa yao
samaki waliokwisha kuvuliwa
 Mwenyekiti wa Ludewa Ash-tech Group Bw.Deogratius Sanga akionesha samaki wanaopatikana katika Mabwawa yao
vijana wa Ludewa Ash-tech group wakiendeleza uchimbaji wa mabwawa mengine ya samaki 






Vijana wa wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe wameamua kuachana na tabia ya kucheza mchezo wa pool nyakati za machana na kuanzisha vikundi vya uwekezaji ikiwa pamoja na ufugaji wa Samaki,Nyuki,Uchimbaji wa visima pamoja na upandaji miti ikiwa ni lengo la kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli katika kujiinua kiuchumi.


Hayo yamesemwa leo wilayani hapa na mmoja wa vijana hao ambaye ni Mwenyekiti wa Ludewa Ash-tech group Bw.Deogratius Sanga alisema kuwa katika kikundi hicho kuna vijana 1o wakiwemo wakike 3 na wakiume 7 ambao awali walikuwa wakijihusisha na michezo ya pool na kusahau miradi yao ambayo waliianzisha ikiendelea kufa.


Bw.Sanga alisema kuwa kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2011 lakini usajiri kamili kimesajiriwa mwaka 2016 kikiwa na malengo ya uelimishaji kwa jamii hasa vijana katika uhifadhi wa mazingira ikiwemo upandaji wa miti,ufugaji wa Nyuki,ufugaji wa Samaki na uchimbaji wa visima lakini katika malengo hayo yote waliweza kufanikisha machache na kuendelea starehe za mitaani ikiwemo uchezaji pool.


Alisema kuwa mpaka sasa Ludewa Ash-tech group wameweza kufanikisha katika ufugaji wa nyuki kuwa na mizinga 46,wameweza kuchimba visima 54 katika makazi ya watu,wamepanda miti ekali 12 na kuwa na mabwawa mawili ya Samaki lakini miradi hiyo yote ilikuwa katika hali mbaya kutokana na kutokuwa na uendelezaji lakini kwa kauli ya Mh.Rais wamepaswa kurudi katika miradi yao na kuiendeleza.


“Ludewa Ash-tech group kama tungeendelea na utaratibu wetu wa zamani tungekuwa mbali kimaisha lakini kutokana na kauli ya Rais wetu imetubidi kurudisha kikundi chetu na kufanya kazi ambazo vijana wote wa Tanzania wanapaswa kutuiga kwani tumefika katika mabwawa yetu ya Samaki tumekuta kunasamaki wakubwa mno hivyo imetupa moyo na tumeanza kuchimba mabwawa mengine tena ili kujipatia kipato”,alisema Bw.Sanga.


Bw.Sanga alisema kuwa vijana wengi nchini wanahitaji msukumo wa viongozi wa juu wa kitaifa kwani kwa kutofanya hivyo wataendelea kufanya starehe huku wazee ndio wakiwa wazalishaji mali hivyo aliwataka vijana kutumia nguvu zao katika kuzalisha na sio kushinda vijiweni na kucheza pool nyakati za mchana.


Aidha katibu wa Ludewa Ash-tech group Bw.Salvius Mwanyika alisema kuwa jambo linalowakatisha tamaa vijana kushindwa kutumia nguvu zao mashambani ni ukosefu wa mitaji kwani wao awali waliweza kuchangishana fedha kwaajili ya kununua vifaranga wa Samaki na mbegu za miti ambapo waliziwatika mbegu hizo za miti na baadae kuipanda miche katika mashamba ya urithi.


Bw.Mwanyika alisema kuwa mpaka sasa wameweza kupanda miti katika ekali 12 na kuwa na mizinga ya Nyuki 46 hiyo yote kutokana na kila mmoja wao kujitolea na sio ufadhiri kutoka kwa wahisani hivyo amewaomba wadau mbalimbali kuliunga mkono kundi hilo ili liweze kutoa elimu kwa vijana wengine ambao bado wako vijiweni.


Alisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa eneo au Ardhi ya kufanyia miradi yao hivyo ameiomba Serikali kuwaunga mkono katika hilo ili waweze kuzalisha samaki wengi  ambao wataweza kuwainua kiuchumi wao na familia zao ambazo zinawategemea.


Mwisho.


No comments: