Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

March 11, 2016

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AWAFUNDA WANALUDEWA.


Dkt.Suzan Kolimba akiongea na wanawake wa Ludewa

 Dkt.Suzan akikumbatiana na diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monika Mchilo
kiongozi wa soko la samaki Ludewa mjini AKIMSHUKURU Dkt.Suzan
Anayecheka ni mbunge mstaafu na mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ludewa Bw.Stanley Kolimba,katikati ni mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya na aliyevaa shati ya kijani ni katibu wa ccm wilaya ya Ludewa Bw.Lusiano Mbosa







Naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje ya nchi na ushirikiano wa Afrika mashariki mabaye pia ni mbunge wa viti maalum katika mkoa wa Njombe Dkt.Suzan Kolimba amewataka wananchi wa wilaya ya Ludewa na mkoa wa Njombe kwa ujumla kwenda na kasi ya utendaji kazi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ili kujinasua na umasikini ulio kithiri.




Dkt.Suzan aliyasema hayo hivi karibuni wakati wakitimiza ahadi yake ya ukarabati wa soko la samaki wilayani Ludewa ambapo alitoa rangi lta miamoja na arobaini pamoja na saruji mifuko ishirini ili kuweza kulikarabati soko hilo ambalo kwa muda mrefu lilisahaulika hali ambayo ilileta sura mbaya ya mji wa Ludewa.




Aliwataka wananchi wote kwa umoja wao kuchapa kazi za kilimo na ufufugaji kutokana na wilaya ya Ludewa kuwa na ardhi nzuri kwaajili ya kilimo na ufugaji kwani kwa kufanya hivyo umaskini uliokithiri wilayni hapa utaondoka mara moja hasa wanawake ambao ndio walezi wa familia ndio ambao pia hufanya biashara ya samaki nyasa katika soko hilo la samaki.




Dkt.Suzan alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Ludewa wanasifika katika utendaji kazi na ndio wilaya pekee katika mkoa wa Njombe inayozalisha zao la mahindi na maharage kwa wingi hivyo wakati umefika sasa hata kwa wanasiasa kuwa na maneno kidogo kazi zaidi ili kuwakwamua wananchi kiuchumi hasa wananchi walioko vijijini.




“Napenda kuwakumbusha wananchi wa wilaya ya Ludewa hasa akina mama wenzangu kuwa tufanye kazi na tutumie kaulimbiu ya maneno kidogo kazi zaidi ili kujiletea maendeleo kwani licha ya mimi kukamilisha ahadi yangu ya ukarabati wa soko hili la samaki ambalo akina mama ndio wafanyabiashara wakuu pia nawahimiza tujikite katika kilimo ambacho ni mkombozi wa maisha ya walio wengi”,Alisema Dkt.Suzan.




Alisema kutokana na utendaji mzuri wa Rais Dkt.Magufuli ni dhahili maendeleo yenye tija yatawafikia wananchi wote hadi wale waliokatishwa tamaa na ugumu wa maisha kule vijijini hivyo wananchi wanapaswa kuliombea Taifa na kumuombea Rais pia kumuunga mkono katika mambo mazuri anayoyafanya kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na umaskini.




Akishukuru kwa utekelezaji wa ahadi hiyo ya Naibu waziri Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monika Mchilo alisema kuwa ni jambo lisilo pingika kuwa utendaji wa viongozi wakuu wanchi unatia moyo hali inayowafanya wananchi nao kujikita zaidi katika uzalishaji kwani kila mmoja anaona na sio kusikia tu utendaji huo.




Mh.Monika alisema kuwa ukarabati wa soko hilo utailetea heshima wilaya ya Ludewa pamoja na wafanyabiashara ambao idadi kubwa ni akina mama wanaofanya biashara ndani ya soko hilo hivyo hawana la ziada zaidi ya kuwaunga mkono viongozi wakuu wanchi kufanya kazi kwa bidii katika kila sekta.




Mwisho.




No comments: