Filikunjombe na Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Rehema Nchimbi wakitoa vifaa mbalimbali kwa mgonjwa hospitari ya wilaya ya Ludewa
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Rehema Nchimbi akigawa chakula kwa wagonjwa
Deo Filikunjombe akila chakula na wagonjwa pamoja na wauguzi
wauguzi wakishiriki chakula
Dkt.Nchimbi akila chakula na mgonjwa katika wodi ya wazazi
Mbunge wa jimbo la Ludewa kupitia chama cha mapinduzi Deo Filikunjombe katika kuazimisha sherehe za Pasaka jana aliweza kuandaa chakula na kula na wagonjwa wa Hospitari ya wilaya ya Ludewa pamoja na kuwagawia wagonjwa hao na wauguzi vitu mbalimbali vikiwemo sabuni na mafuta ya kupaka.
Utaratibu wa kula chakula na wagonjwa ni utaratibu aliyojiwekea kila mwaka tokea alipopata nafasi hivyo hivyo kila mwaka amekuwa akikila na wagonjwa katika hospitari mbalimbali katika kata na vijiji vya wilaya yake na kupata kuongea na wagonjwa pamoja na wauguzi ili kupata changamoto zinazowakabili katika Sekta ya Afya.
Katika chakula hicho Filikunjombe aliweza kushiriki na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Rehema Nchimbi ambaye alifurahishwa kwa mtaratibu huo wa kuwafariji wa kwanjwa kwani kuna baadhi ya wagonjwa hukaa muda mrefu mawodini bila kutembelewa na viongozi wa kisiasa wala Serikali hali ambayo inawakatisha tamaa ya kuendelea kuishi.
Dkt.Nchimbi aliitaka Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuandaa mpango wa chakula kwa wagonjwa hasa katika wodi ya wazazi ambao akina mama wajawazito hufika kutoka vijiji na kukaa hapo wakisubiri tarehe ya kujifungua.
Alisema akina mama wengi wamekuwa wakikosa lishe kutokana na kushindwa kuelekezwa kwa vitendo hivyo Halmashauri inapaswa kutenga bajeti au kutafuata wafadhiri watakaoweza kuchangia mpango huo wa chakula kwa akinamama hao ambao afya zao ziotaboreka na kupata elimu ya kula chakula bora wawapo majumbani kwao.
“Nakuagiza mkurugenzi kuandaa mpango wa chakula ambao utawawezesha wazazi wanaosubiria muda wao wa kujifungua kupata chakula bora hapa namimi kwa kuanzia natoa gunia tano za mahindi ili kuanza mpango huu pia nakuomba Mh.Filikunjombe kuunga mkono kwa kuchangia mpango huu”,alisema Dkt.Nchimbi.
Filikunjombe alisema kuwa huo ni utaratibu wake wa kula na wagonjwa kila mwaka hivyo aliwataka wauguzi kufanya kazi kwa bidii kwani kazi hii ni wito hivyo yawapasa kuonesha upendo kwa wagonjwa wanaowahudumia ili Hospitari ya wilaya iwe ya mfano tofauti na wilaya nyingine.
Alisema Hospitari ya wilaya ya Ludewa ni Hospitari pekee inayotegemewa na wawekezaji katika miradi mikuwa inayotarajia kuanza ya makaa ya mawe ya Nchuchuma na kile chuma cha Liganga hivyo wauguzi wanapaswa kujiandaa kwa kuongeza elimu na ujuzi zaidi ili kukabiliana na uwingi wa watu wanaotarajia kuja.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment