Filikunjombe akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kujiandikisha na kukabidhiwa kitambulisho mwenye miwani ni kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Prof.Amone Chaligha
Filikunjombe akiweka alama za vidole katika mashine ya uandikishaji
Mbunge wa
jimbo la Ludewa kupitia chama cha mapinduzi katika mkoa wa Njombe Deo
Filikunjombe amewataka wananchi wa wilaya ya Ludewa kujiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura ambalo limeanza leo tarehe 16/3/2015 ili
kuweza kupata fulsa ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu
unaotarajia kufanyika ockoba mwaka huu.
Filikunjombe aliyasema hayo jana katika kituo cha uandikishwaji wapiga kura katika shule ya msingi Ludewa mjini wakati akijiandikisha ikiwa ni siku ya ufunguzi wa undikishwaji ulioanza rasmi wilayani hapa na kuwataka wananchi kuachana na maneno ya kizushi ya baadhi ya wanasiasa wanaowarubuni wananchi kutojiandikisha.
Alisema kuwa kwa wananchi wa Ludewa vitambulisho hivyo vitatumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya kusajilia simu na mengineyo hivyo hakuna haja ya kukaa kuwasikiliza wasio na mapenzi mema na nchi yao kwa kuwazuia wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba.

“Mimi kama
mbunge wajimbo la Ludewa leo nimejiandikisha na tayari nimesha kipata
kitambulisho change cha kupigia kura hivyo nawaomba wananchi wangu kujitokeza
wote bila kukosa ili kuweza katika kufanikisha zoezi hili wani kitambuisho cha
mpiga kura kitawasaidia kwa mambo mengi,msiwasikilize wazushi nisikilizeni mimi
ambaye mliniamini na mkanichagua kuwa mwakirishi wenu”,alisema Filikunjombe.
Alisema kama
mtanzania unapaswa kujiandikisha na kutumia haki yako ya kikatiba katika
kuipigia kura ya ndiyo katiba mpya inayopendekezwa pia kuchagua viongozi
mnaowataka ifikapo oktoba mwaka huu.
Aidha
kamishna wa tume ya Taifa ya uchaguzi Prof. Amone Chaligha akijubu swali la
waandishi wa habari kuhusiana na kasoro za mashine za BVR alisema awali
kulikuwa na kasoro za kutosoma kwa baadhi ya watu lakini wataalamu wa mifumo ya
Komputor wameshairekebisha hivi sasa hakuna tatizo tena.
Prof.Chaligha
alisema kinachotakiwa ni wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani
zoezi hilo wilayani Ludewa litafanyika kwa muda wa siku saba na baada ya hapo
zoezi litahamia maeneo mengine hivyo hakuna haja ya kuchelewa kujiandikisha.
Alisema
tokea zoezi hilo lianze wilayani hapa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza kama
ilivyokuwa mji wa Makambako hivyo kila mwananchi anatakiwa kutumia fulsa hii ya
kujipatia kitambulisho chake sasa ili kuweza kutumia katika upigaji kura.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment