Wananchi
wa kata ya Ludende wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameitupia lawama
Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwa kushindwa kuikarabati barabara inayotoka kata
ya Milo kupitia Ludende hadi Ketawaka hali inayosababisha kubeba maiti kwa
kutumia pikipiki amaarufu kama bodaboda.
Akiongea
kwa hisia kali mmoja wa wananchi wa kata hiyo aliyejitambulisha kwa jina la
Peter Mgimba amesema ni muda mrefu mpaka sasa wamekuwa wakiahidiwa kuhusiana na
ukarabati wa barabara hiyo jambo ambalo limebaki ni kitendawili.
Bw.Mgimba
amesema katika kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa Mwenyekiti wa
Halmshauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Mathei Kongo aliweza kuahidi kuwa baada ya
siku tano barabara hiyo ingefanyiwa matengenezo lakini mpaka sasa ni mwezi
mmoja umepita hakuna jambo linalofanyika.
Bw.Mgimba
anasema kijiji cha Ludende ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao ya
mahindi,alizeti na mbao lakini uwezekano wa kuyasafirisha mazao hayo hadi
sokoni ni mgumu kutokana na ubovu wa barabara hali hiyo ni mbaya zaidi
inapelekea kuwabeba wagonjwa katika machela na maiti katika bodaboda umbali wa
kilomota 15 kutoka kijiji cha Ludende hadi hospitari ya Milo.
“Tunapata
shida sana na ubovu wa hii barabara kwani tumechoshwa na ahadi za viongozi wa
Halmashauri,tumekuwa tukiishi maisha ya ajabu kwani mpaka leo tunasafirisha
maiti kwa kutumia bodaboda kwa umbali wa kilomita 15 kwa kiasi cha shilingi
laki moja jambo ambalo si haki kama wananchiwa Tanzania”,alisema Mgimba.
Alipojaribu
kutafutwa kwa njia ya simu ya kiganjani Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Kongo ili
aweze kujibia jambo hilo hakuweza kupatikana lakini juhudi za kumtafuata
zinaendelea ili aweze kutoa majibu ya ahadi yake ambayo aliwaahidi wananchi wa
kata ya Ludende.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment