Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

December 17, 2013

WAKALA WA NISHATI YA UMEME VIJIJINI REA WAAHIDI KUWA BEGA KWA BEGA NA WADAU WA UMEME VIJIJINI

 Afisa Uhusiano wa REA Bi.Jaina Msuya Akizungumza Wakati wa Kufunga Mafunzo Hayo Yaliyofanyika Katika Ukumbi wa
Nazareth Center Mjini Njombe.






Baadhi ya Wadau wa Nishati ya Umeme wa Maporomoko ya Maji Nchini Wakifunga Mafunzo ya Wiki Mbili Yaliyofadhiliwa na REA




Serikali Imesema Itaendelea Kuwajengea Uwezo na Kuwawezesha Wadau wa Nishati ya Umeme wa Maporomoko Ya Maji na Kuhakikisha Inatimiza Lengo la Kuongeza Idadi ya Watanzania Wanaopata Huduma ya Nishati ya Umeme Hadi Kufikia Asilimia 30 Ifikapo Mwaka 2015.

Aidha Serikali Imesema Itaendelea Kushirikiana na Taasisi Mbalimbali Zikiwemo za Dini,Mashirika Binafsi na Watu Mbalimbali Wanaojihusisha na Sekta ya Nishati kwa Lengo la Kuongeza Kiwango Cha Uzalishaji wa Umeme Hapa Nchini.

Akizungumza Wakati wa Kufunga Mafunzo ya Wiki Mbili Kwa Wadau wa Nishati ya Umeme wa Maporomoko ya Maji Yaliyokuwa Yakifanyika Mjini Njombe Mwakilishi wa REA Bi.Jaina Msuya Amesema Upatikanaji wa Umeme wa Uhakika Utasaidia Kukuza Uchumi Hasa Katika Maeneo ya Vijijini.

Akisoma Risala Kwa Niaba ya Washiriki wa Mafunzo Hayo Mmoja wa Washiriki Bw Moshi Shaaban Amesema Kupitia Mafunzo Hayo Wameweza Kujifunza Mambo Mbalimbali Yatakayosaidia Kupunguza Baadhi ya Changamoto Zilizokuwa Zikiwakabili.

Aidha Amesema Kuwa Kutoka na

Mafunzo Hayo Wameamua Kuanzisha Umoja wao Kitaifa Utakaofanya Kazi ya Kuchochea na Kuihamasisha Serikali Kuwasaidia Kupata Misaada Mbalimbali ya Kuendeleza Miradi Yao.

Akifunga Mafunzo Hayo ya Wiki Mbili Kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe,Afisa Kilimo na Umwagiliaji Katika Halmashauri Hiyo Bi.Elitha Mligo Amewataka Wadau Hao Kuhakikisha Wanatekeleza Kwa Vitendo Mafunzo Waliyoyapata Kwa Kufanikisha Azma yao ya Kusogeza Huduma ya Nishati Kwa Wananchi Vijijini

Aidha Amewataka Kutumia Fursa Hiyo ya Kuunda Umoja Wao Katika Kuhakikisha Serikali Kupitia REA Inawaunga Mkono Kwa Asilimia Kubwa Pamoja na Kuhakikisha Wanasajili Umoja Wao Ili Uwasaidie Katika Miradi Yao

Mafunzo Hayo Yalianza Tangu Disemba 4 Mwaka Huu Ambayo Yalikuwa Yakifanyika Katika Ukumbi wa Nazareth Mjini Njombe Kwa Kuwakutanisha Zaidi ya Wadau 30 wa Nishati ya Umeme Huo Kutoka Katika Mikoa Mbalimbali Hapa Nchini.


 Na  Gabriel  Kilamlya Njombe

No comments: