Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

November 13, 2013

GONJWA LA UKIMWI NA SABABU ZA UENEAJI MKOANI NJOMBE.




Unaposema UKIMWI hakuna mtu hata moja nchini hususani mkoa wa Njombe anayeweza kuhoji ni kitu gani zaidi ya kisikitika kutokana na ugonjwa huo kukatisha maisha ya watanzania kila kukicha na kila familia imeshakumbwa na janga hilo.

Nasema janga kwa kua hakuna familia hata moja nchini Tanzania ambayo haijafikwa na msiba huu kwa ndugu wa jirani hata rafiki wa mbali ambaye aliwahi kufa kutokana na kukumbwa na janga hili linalowatesa wataalamu ambao mpaka sasa wanaumiza vichwa ili kupata ufumbuzi wa dawa ya gonjwa hili.

UKIMWI ni kifupi cha upungufu wa kinga mwilini unaosababishwa na kuwepo kwa virusi cha ukimwi  mwilini ambayo vinaharibu mfumo wa utengenezaji wa kinga za mwili,katika hatua hii mtu huonesha dalili za ugonjwa.

Mtu mwenye ukimwi ni yule ambaye mwili wake umedhohofishwa na VVU yakichangiwa na magonjwa mbalimbali tegemezi lakini mtu huyo huumwa na kuonesha dalili mbalimbali za magonjwa.

Ikumbukwe kuwa kunautofauti mkubwa wa VVU na UKIMWI na maaana halisi ni kama ifuatavyo,VVU ni virus vya ukimwi ambapo mtu anaweza kuishi na virusi vya ukimwi bila ya kuonesha dalili za magonjwa na UKIMWI ni ugonjwa tayri mtu huonesha dariri na kudhoofu.

Katika mkoa wa Njombe takwimu za maambukizi kitaifa ziko juu kwa 14.5% ukilingabisha na mikoa mingine nchini hali ambayo imekuwa ikirudisha maendeleo chuma kuanzia ngazi ya familia na hata jamii kwa ujumla ukilinganisha na maeneo mengine.

Mkoa wa Njombe wenye hali ya baridi kali katika maeneo ya wilaya za Makete,Njombe,Wanging’ombe na Ludewa na kuwa na pombe ya asili aina ya Ulanzi baadhi ya watu wanasema ndio sababu kubwa ya kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi.

Kutokana na sababu hizo bado utafiti unaendelea sababu kuu za kuenea kwa kasi katika mkoa huo na kuwa na sifa ya kuwa mkoa wa kwanza kitaifa katika takwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi na kurudisha maendeleo ya wananchi wa mkoa huo nyuma.

Kuna mazungumzo mengi ya wataalamu mbalimbali na wasio wataalamu wa masuala ya afya yanayobainisha chanzo cha ukimwi lakini mpaka sasa hakuna aliyewahi kuthibitisha chanzo hicho ambayo kila mtu ana hamu ya kujua ukimwi ulitokea wapi na ulianzaje.

Watu wengine wanasema kwamba virusi vya ukimwi vilitengenezwa katika maabara na wengine wanasema vil;ikuwepo tangu zamani katika sehemu ya misitu ya Afrika ya kati na kutokana na mwingiliano wa nyani na binadamu viliweza kuenea,ukweli ni kwamba uhakika kuhusu chanzo cha ukimwi hakijulikani.

Hata hivyo hakuna umuhimu sana wa kufahamu ugonjwa huo ulitoka wapi na nani ni mgunduzi bali jambo la msingi ni kuhafamu kwamba ugonjwa huo upo katika mikoa yote Tanzania na kwamba lazima tujikinge kwa sababu hakuna tiba wala chanjo.

Sababu kuu za kuenea kwa maambukizi ya gonjwa hili la ukimwi ni ngono zembe yaani kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja na kuacha uaminifu kwa mwenzi wako hali hii inadhihirisha kuwa mtu akiwa na wapenzi wengi uwezekano wa kuambukizwa unaongezeka.

Hivyo kutokana na idadi kubwa ya wapenzi inaweza kuwa chanzo cha kupata virusi,vilevile mtu akifanya mapenzi yasiyo salama yaani kuingiliana kimwili bila kutumia kondomu anahatarisha maisha yake.
Pia kuchelewa kutibu magonjwa mengine ya zinaa inachangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI kwa mfano kama mtu anaugua ugonjwa wa zinaa vijidudu vya vya ukimwi vinaweza kuingia mwilini kwa urahisi zaidi kwa sababu ya vidonda sehemu zake za siri.

Matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na pombe yanaweza kuchangia kufanya maamuzi yasiyo sahihi katika matendo ya ngono hasa katika vijiji vya mkoa wa Njombe ambapo bado jamii haijaelewa vema matumizi ya kinga.

Tuiangalie wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe kwa mapana zaidi katika suala la gonjwa hili la UKIMWI kabla ya kuja waekezaji wa migodi ya makaa ya mawe Mkomang’ombe na chuma cha Liganga mwaka 2014.

Katika wilaya za Mkoa wa Njombe wilaya ya Ludewa ni moja ya wilaya yenye maambukizi ya juu kwa takwimu za wataalamu ni 6% na idadi ya wakazi wa wilaya ya Ludewa hawazidi laki moja lakini maambukizi yake ni makubwa zaidi.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha ameweza kuwatahadharisha wananchi wa wilaya yake kuwa kupitia wageni watakao kuja kufanya kazi wilayani humo maambikizi ya ukimwi yanaweza kuongezeka kama hakutakuwa na juhudi za maksudi za kujizuia na tabia zisizo faa.

Bw.Madaha anasema miradi hiyo ni mizuri kwa maendeleo ya Taifa na jamii ya watu wa wilaya ya Ludewa lakini inaweza kugeuka kuwa karaha kwa wananchi wasiojiheshimu na kutoheshimu wapenzi wao na kuishia kufa na ukimwi.

Alizitaja sababu kubwa wilayani mwake za kuenea kwa ukimwi ni ngoma za usiku pombe za kienyeji zikiwemo za ulanzi na komoni,vituo vya meli hasa mwambao wa ziwa Nyasa wasafiri wengi hulala mchangani wakisubiri kusafiri usiku kutokana na meli hizo kupita katika vituo vya wilaya ya Ludewa usiku.

Sababu nyingine ni wananchi kutokana na uchache wao na kufahamiana husababisha kupapalika na wageni wanaoingia wilayani humo kwa kutokujua walikotoka na afya zao zikoje hivyo hujirahisisha na kufanya nao matendo ya ngono.

Alisema imeshazoeleka kuwa maeneo ya migodi ndio maambukizi ya ukimwi huenea kwa kasi kutokana na mkusanyiko mkubwa wa watu lakini katika mkoa wa Njombe wananchi wanatakiwa kutahadharishwa mapema kabla ya wawekezaji hawajaanza kuajiri wafanyakazi wengi katika miradi iliyoko Ludewa.

Aidha wanaotakiwa kuihabarisha jamii umuhimu wa kutokuwa na wapenzi wengi ni taasisi mbalimbali za kiraia,vyombo vya habari na Serikali ili wananchi wa mkoa wa Njombe waweze kunufaika na fulasa zitokanazo na migodi na si kuangamia na janga la Ukimwi.

Hivi karibuni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliweza kufanya ziara katika mkoa wa Njombe kwaajili ya uzinduzi wa mkoa huo na kuzitembelea wilaya zake ni mkoa ambao takwimu za maambukizi ya ukimwi yako juu kuliko mikoa mingine nchini.

Dkt.Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mkoa wa Njombe aliweza kuwaeleza wananchi kuwa ukimwi umekuwa tishio kubwa Duniani na bado dawa haijapatikana hivyo kila mmoja anatakiwa kuwa makini na mwenzi wake.

Alisema imekuwa kama utamaduni wa baadhi ya watu kupuuza habari wanazopewa na wataalamu na kuona kama hakuna hakika ya takwimu zinazotolewa na wataalamu hali inayofanya watu hao kuendelea kurithi wajane na kutokuwa waaminifu kwa wapenzi wao.

Dkt.Kikwete alisema suala la kuwa mkoa wa Njombe kuongoza katika maambukizi ya Ukimwi sio  sifa ya kujivunia kutokana na sifa hiyo kuwa mbaya hivyo kula mwananchi wa mkoa wa Njombe anatakiwa kuwa makini na afya yake.

Aliwataka wananchi kuwa wastaarabu kwani suala la kujamiiana halina dharula kutokana na kila mtu hukubaliana na mwenzi wake na kupanga muda wa kukutana hivyo inapaswa kujiandaa kwa kuwa na kinga ili kupunguza maambukizi hayo.

Dkt.Kikwete aliweza kuwasifu baadhi ya wanaume ambao wameweza kuingia katika mpango wa kufanyiwa tohara kwani imethibitishwa kitaalamu kuwa kunauwezekano mkubwa wa kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Akitolea mfano katika mikoa ambayo ilikuwa na tamaduni na mila ya kufanyiwa tohara ya kitabibu kwa wanaume Dkt.Kikwete alisema mikoa hiyo ni kama Tanga, Kilimanjaro, Mtwara na Arusha maambukizi ya virusi vya ukimwi yamekuwa chini hivyo aliwataka wanaume wote Mkoani Njombe bila kujali umri wajitokeze katika kupata huduma ya tohara ya hiari katika vituo vya afya.

Alisisitiza kuwa Tohara ya hiari ya kitabibu kwa wanaume inaweza kumkinga mwanaume kwa 60% hivyo asilimia 40% zilizobaki ni kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako, kutumia kondomu au Kuacha kabisa kushiriki ngono.

Alisema Tanzania bila ukimwi inawezekana kutokana na kama kila mmoja wetu atachukua tahadhari mapema kama haiwezekani kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu basi watu wanapaswa kutumia kinga ili kutopingia katika janga hili linalorudisha maenendeleo ya taifa nyuma.

Vijidudu vya ukimwi vinapatikana wapi? Vijidudu vya ukimwi vinapatikana katika majimaji yaliyoko mwilini hasa sehemu za siri hivyo ni rahisi kuambukizwa ukimwi kama unamchubuko ambapo majimaji hayo yenye virusi yatapita katika michubuko ya mtu mwingine.

Hivyo kama kila mtanzania atachukua tahadhari ya kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu na akishindwa anashauriwa kutumia kinga ili kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi kwa urahisi zaidi na kwa wanaume wnashauriwa kufanyiwa tohara itakayowasaidia kupunguza maambukizi.

Mwisho.

No comments: