Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

November 26, 2013

ASKOFU JOHN SIMALENGA WA ANGLIKANA DAYOSISI YA NJOMBE AFARIKI DUNIA


Pichani  ni Askofu John Simalenga wa Dayosisi ya Njombe Kanisa la Anglikan Amefariki Dunia Asubuhi ya Saa Kumi na Moja Novemba 24 Mwaka Huu na Mazishi Yanatarajiwa Kufanyika Novemba 28 Katika Kanisa Hilo.


Taarifa Toka Kwa Msaidizi wa Askofu Huyo Mchungaji Canon Mlelwa Amesema Kuwa Marehemu Simalenga Amefariki Dunia Baada ya Kuugua Kwa Kipindi Kifupi Kwa Ugonjwa wa Malari na Kisukari Alichogundulika Kuwa Nacho na Hivyo Hadi Kifo Kinamkuta Alikutwa na Malari Mbili.

Aidha Mlelwa Amesema Kuwa Marehemu Askofu Simalenga Amekufa Akiwa na Miaka 60 Ambapo Alizaliwa Mwaka 1953 Katika Kijiji cha Milo Wilayani Ludewa na Uaskofu Alipata Julai 7 Mwaka 2007 Kisha Kuwa Askofu wa 7 Wa kanisa Hilo.

Katika Hatua Nyingine Askofu Simalenga Ameacha Watoto Wanne na Mjane Mmoja.

Na Gabriel Kilamlya,Njombe

No comments: