MKUU wa Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe Juma Madaha jana aliongoza Madiwani wote, wakuu wa
idara, wananchi na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa sherehe za upandaji miti
kiwilaya katika kijiji cha Madindo kata ya Ludende na kufanikiwa kupanda Ekari
kumi sawa na miche zaidi ya 5450.
Akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo Bw. Madaha
alisema maadhimisho haya kitaifa yatafanyika April mosi mwaka huu lakini Ludewa
yamefanyika januari 14 kwa kuzingatia hali halisi ya msimu wa mvua katika
maeneo mengi ya wilaya hiyo.
‘’’’ sisi kupanda miti leo
ni muda muafaka kabisa kulingana na hali ya hewa ya huku kwa sababu
tukisema tungoje mpaka tarehe ya kupanda miti kitaifa mvua kwetu zitakuwa
zinaelekea kukatika kwa hiyo upandaji huo utakuwa hauna tija.’’’’ Alisema Bw.Madaha.
Aidha Bw.Madaha akaongeza kuwa wilaya yake imeotesha miche
zaidi ya milion 4 kwa ajili ya kupanda msimu huu, ambapo kata ya Ludende pekee
miche 221,974 imeoteshwa na watu binafsi, vikundi, taasisi na mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali na kuzitaka kata zingine zenye mwamko mdogo kujifunza
ili kujiletea maendeleo yao.
‘’’’ ndugu wananchi leo ni siku ya uzinduzi wa upandaji miti
kiwilaya, hii ina maana kuwa upandaji wa miti ulishaanza na utaendelea baada ya hapa mpaka hapo mvua zitakapokaribia
kukatika, Kila mwananchi anatakiwa kujiwekea malengo ya kupanda miti ya kutosha
ili kufikia lengo.’’’alisisitiza Bw.Madaha.
Naye Fidelis Lumato
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa akawataka wananchi kuacha
tabia ya kuchoma moto hovyo na kuacha kutegemea kilimo cha mazao ya mahindi
pekee katika kujikwamua na umaskini badala yake wageukie upandaji miti na
kutumia mazao ya mbao kujiondoa kwenye wimbi la umaskini wa kipato kwani miti
haihitaji pembejeo.
Bw.Kimato akaongeza kuwa mkakati wa kupunguza umaskini
hauwezi kufanikiwa bila kuzingatia suala la kuhifadhi mazingira kwa kuwa wilaya
bado ina uoto mzuri wa asili kwasababu misitu ya asili haijaharibiwa
ukilinganisha na maeneo mengine nchini.
Uharibifu wa mazingira unaoikabili wilaya ya Ludewa ni pamoja
na uchomaji miti, na misitu unaosababisha mmomonyoko wa udongo na mafuriko,
kulima kwenye vyanzo vya maji na mabonde chepechepe ambapo matokeo yake ni
kukauka kwa vyanzo ya maji miche na chemichemi.
Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Afisa ardhi na mali asili
wilaya ya Ludewa Gilbert Ngailo alisema lengo la kufanyia uzinduzi wa kupanda
miti katika kata ya Ludende ni kutokana na hamasa na mwitiko walionao wananchi
wa kata hiyo hasa kwenye suala la upandaji miti ambapo kila mwananchi ana ekari
zaidi ya moja.
‘’’’ dawa ya kukomesha uharibifu wa mazingira ikiwemo
uchomaji moto kichaa itapatikana muda si mrefu ambapo halmashauri itaunga
sheria ndogondogo kwa ajili ya kumtaka kila mwananchi kupanda miti kwa kiwango
cha kima cha chini ekari mbili kufanya hivyo kila mtu atakuwa mlinzi wa
mwenzake.’’’’ Alisisitiza Ngailo.
Ngailo aliyataja maeneo mengine yenye mashamba ya miti ya
halmashauri kuwa nipamoja na shamba la miti lenye ekari 20 za miti ya
mikaratasi ambayo tayari imeanza
kuvunwa,Mlangali yenye miti hekta 61 aina ya milingoti na ekari 10, kijiji cha
Ilininda ekeri 10, Utiriri ekari 10 na madindo ekari zaidi ya 102 sawa na hekta
40.
mwisho
No comments:
Post a Comment