Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

December 15, 2012

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUHAMASISHA MAENDELEO KWA WAAMINI WAO


Viongozi wa Dini,Siasa na Watendaji wa Serikali Wamelaumiwa Kwa Kushindwa Kuhamasisha Wananchi Kuhusu Umuhimu wa Kuchangia Mradi wa Maji Kutoka Mto Nyenga Hali Iliosababisha Mradi Huo Kwenda Katika Hali ya Kusuasua Hadi Kufikia Sasa.

Badala Yake Wametakiwa Kuchukua Hatua za Kuhakikisha Wananchi Katika Maeneo Yao Wanapata Taarifa Sahihi Kuhusu Mradi Huo na Jinsi Utakavyowapunguzia Tatizo la Maji Ambalo Limekuwa Sugu Kwa Sasa Katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Njombe.

Mzee Edwin Kilasi ni Katibu wa Kamati Maalum Inayosimamia Ujenzi wa Mradi Huo Amesema Hali Hiyo Imesababisha Michango Kwenda Katika Hali Isioridhisha Ambapo Hadi Kufikia sasa Jumla ya Fedha Zilizokusanywa ni Shilingi Millioni 12.6 Kati ya Shilingi Billioni Mbili Zinazohitajika Kukamilisha Mradi Huo
 

Akizungumzia Malalamiko ya Wananchi wa Kata ya Ramadhani ya Kutopata Elimu Kuhusu Mradi Huo Amesema Wananchi Hao ni Vema Wakashirikiana na Viongozi Wao Kwa Kuandaa Mkutano Ili Kamati Hiyo Iweze Kwenda Kutoa Elimu
 

Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Ramadhani Bw Bashir Sanga Amesema Hadi Kufikia Sasa Hakuna Mwananchi Hata Mmoja Aliechangia Licha ya Uongozi wa Mtaa Kupokea Vitabu Vya Michango Kwa Zaidi ya Mwezi wa Pili Sasa

Mradi wa maji wa mto nyenga uliibuliwa na wananchi wenyewe ambao kwa pamoja walipendekeza viongozi wa dini kusimamia mradi huo kwa madai ya kuwa hawana imani na viongozi kutoka serikalini huku zoezi hilo likionekana kuendelea kuwa gumu kwa viongozi hao wa kiroho kutokana na hamasa ndogo ya wananchi kuchangia.

No comments: