Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

November 17, 2012

NYUMBA ZA POLISI WILAYA YA LUDEWA ZATELEKEZWA

NDOTO na furaha za wananchi na askari polisi wilayani Ludewa katika mkoa wa njombe kuhusu ujenzi wa kituo kipya pamoja na nyumba za watumishi zimetoweka kutokana na majengo hayo kutelekezwa zaidi ya miaka minne bila kukamilika.

 Aidha majengo hayo badala ya kuishi askari sasa yamekuwa magofu na mapango ya kuishi panya na wanyama wengine huku majengo hayo yakigeuzwa madanguro ya kufanyia ukahaba kwa vijana na watu wazima wanaokwepa kutumia nyumba za kulala wageni kwa hofu ya kuonekana na wake zao.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wananchi wanaoishi nyumba moja na askari hao, walisema wamechoshwa na kuishi jirani na walinda usalama hao kutokana na tabia zao za kuwalazimisha raia kufuata amri zao.

 “” tunaomba serikali imalizie ujenzi wa kituo cha polisi pamoja na nyumba za askari ili tuondokane na kero hizi vinginevyo wasijekushangaa siku moja kutokea mapigano kati ya askari wa uraiani na wananchi hususani wamiliki wa nyumba na vibanda vya kupanga.”” Alisema mama Haule mkazi wa kitongoji cha Ibani katika kata ya Ludewa mjini

Wakizungumza kwa masharti ya kutoandikwa majina yao kwa kuwa wao si wasemaji wa jeshi hilo askari polisi wilayani Ludewa waliilalamikia tabia ya jeshi hilo kutelekeza jingo bila sababu ya msingi huku wao wakiendelea kuishi uraiani na kutumia nyumba ya mtu binafsi isiyo na sifa kuwa ndiyo kituo cha polisi jambo ambalo ni hatari kwao na washtakiwa.

“” sisi tunashangaa serikali kujenga vipande vipande, ni wazi na kila mtu anaamini kwamba jengo lolote la serikali linapoanza kujengwa bajeti yake huwa imekamilika kwa kuwa mipango na bajeti vilikwishaainishwa na kupitishwa kwenye vikao halali sasa inakuwaje ujenzi kusimama miaka minne?”” Aliuliza askari mmoja anayeishi nyumba mbovu za kupanga uraiani kutokana na uhaba wa nyumba Ludewa

 Fulgence Ngonyani ni kamanda wa polisi mkoa wa njombe kwa upande wake akasema askari na wananchi wawe watulivu kwa sababu serikali inakabiliwa na ufinyu wa bajeti na kwamba ana imani majengo hayo yatakamilika pindi bajeti itakaporuhusu.

 “” tatizo ni suala la upatikanaji wa fedha bajeti inayotolewa haijatosheleza kuendelea kumaliza hapo hata hivyo sijui gharama ya majengo hayo, ninachojua kuna miradi inakwenda kwa awamu hakuna fedha iliyotengwa moja kwa moja.”” Akaongeza kamanda Ngonyani

CLODWIG MTWEVE ni kamishina wa utawala na usimamizi wa raslimali za jeshi la polisi nchini akasema bajeti ndogo na hali mbaya ya uchumi ndiyo vinavyofanya kuchelewa kwa kumalizika kwa miradi iliyoanzishwa na serikali kwani kila mwaka fedha huidhinishwa kwa ajili ya kumalizia viporo lakini wakati mwingine mambo ya kitaifa yanaingilia inabidi kusubiri tena.

 “” gharama ya mradi inaweza kufahamika nap engine kupangwa kufanyika kwa muda Fulani na ile bajeti hugawanywa kulingana na kila mwaka wa fedha sasa inapotokea majukumu ya kitaifa inabidi miradi mingine isimame lakini naamini katika mwaka wa fedha ujao serikali itaweza kumalizia mradi huo.”” Akasisitiza kamishna mtweve

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kampuni ya MNM engeneering Ltd Joseph Msangi mradi huo mpaka kukamilika utagharimu zaidi ya shilingi 800 milioni.

 mwisho

No comments: