November 17, 2012
JENGO LA MAABARA WILAYA YA LUDEWA LAKATALIWA KUPOKELEWA KWA MKANDARASI
UTATA mkubwa umeibua wilayani Ludewa mkoa wa Njombe jana baada ya jengo la kisasa kwaajili ya Maabala lililojengwa na kampuni ya CSI Costruction kwa msaada wa watu wa Marekani kushindwa kukabidhiwa kwa Halmashauri ya wilaya hiyo.
Jengo hilo limezua utata baada ya wakaguzi kulikagua na kubaini mapungufu yanayotakiwa kurekebishwa yakiwemo ujeni wa tanki la maji kutokana na nguvu ya maji yanayotakiwa kutumika katika maabala hiyo kuwa ndogo.
Hata hivyo msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka kampuni ya CSI Costruction Bw.Hamis Lwambo alikanusha kampuni yake kuwa na mapungufu ya ujenzi wa jingo hilo na kueleza vitu vinavyodaiwa havikukamilika havikuwa katika mkataba.
Bw.Lwambo alisema wafadhiri wa ujenzi wa jengo hilo ambao ni Central Disease Contor(CDC)kwa msaada wa watu wa Marekani katika makubaliano ndani ya mkataba ujenzi wa tanki la maji haikuainishwa hivyo wanahitaji kufanya mazungumazo ya ongezeko la ujenzi huo.
“Kampuni yetu haina makosa kwani leo ilitubidi kulikabidhi jengo hilo kwa uongozi wa Halmashauri baada ya kukaguliwa lakini imeshindikana hata hivyo viongozi wetu watakaa meza moja na uongozi wa CDC ili kukubaliana nini kifanyike ndipo tulikabidhi”,alisema Bw.Lwambo.
Jengo hilo la maabala ya kisasa ambalo limejengwa kwa fedha za kitanzania shilingi milioni mianane lilitarajia kukabidhiwa jana rasmi ni kati ya majengo ya kisasa nchini yanayotarajia kuwa na mitambo ya kisasa ya vipimo kwaajili ya binadamu.
Aidha mganaga mkuu wa wilaya ya Ludewa Dr.Happynes Ndossi alisema ofisi yake imejipanga kulitumia vyema jengo hilo na vifaa vya kisasa vitakavyowekwa humo pindi litakapokabidhiwa rasmi.
Dr.Ndossi alisema wafanyakazi wa Hospitali ya wilaya ya Ludewa walikuwa na shauku ya kukabidhiwa jengo hilo ili waanze kufanya kazi lakini wakaguzi wanataka kuhakikisha jengo hilo linajengwa katika kiwango kinachokubarika na kuwa na mambo yote muhimu yanayohitajika.
Alisema ujenzi wa jengo hilo umefanyika takribani miezi minane mpaka kukamilika kilichobaki ni marekebisho madogo ambayo anauhakika yatakamilika hivi punde ili waweze kukabidhiwa na kulifanyia kazi.
Dr.Ndossi alisema awali kulikuwa na upungufu wa vyumba vya maabala ambapo iliwawia vigumu kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kuokana na uhaba wa vifaa na vyumba lakini ujenzi wa jengo hilo ni ukombozi kwa wananchi wa wilaya ya Ludewa.
Kutokana na ongezeke la watu katika wilaya ya Ludewa maabala hiyo imejengwa kwa muda muafaka ili kukabiliana na ongezeko la wawekezaji wanaotarajia kufanya kazi ndani ya wilaya hiyo.
Dar.Ndossi aliwataka wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Ludewa kuwa wavumilinu kutokana na kutokabidhiwa maabala hiyo kwani marekebisho yakikamilika wataitwaa na kuitumia katika kazi zao.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment