Mpambano mkali umefanyika jana jumapili katika viwanja vya
mpira wa miguu wa Ludewa mjini kati ya timu ya Boma FC kutoka kata ya Milo na
Home Boys ya ludewa mjini katika mchezo wa kirafiki ili kujiandaa na ligi
daraja la pili ngazi ya mkoa.
Timu ya Home boys ya Ludewa mjini ilikubali kipigo cha mabao
mawili kwa moja kwa wasakata kabumbu hao wa Boma FC kutoka Milo ambapo giri la
kwanza lilifungwa na Yohana Mgaya na la pili likafungwa na Frank Vegula ku
kichwa hao wote ni washambuliaji wa timu ya Boma Fc.
Hata hivyo mshambuliaji machachali wa Home Boys aliifungia
timu yake goli la kufutia machozi kwa njia ya penati baada ya beki wa timu ya
Boma kumfanyia madhambi mshambuliaji huyo katika eneo la hatari ambapo mwamuzi
aliamuru iwekwe penati.
Mpaka firimbi ya mwisho wa mchezo huo inapulizwa Boma fc
waliondoka na ushindi wa magori mawili kwa moja ambapo hali hiyo imezidi kuipa
matumaini timu ya boma katika ligi ya daraja la tatu nane bora inayotarajia
kutimua vumbi umamosi katika viwanja vya ludewa mjini.
Katika hatua nyingine timu nne kutoka wilayani Ludewa
zinatarajia kucheza ligi daraja la pili zikishinda na timu za wilaya ya Makete
na Njombe mwishoni wa mwezi huu.
Akizitaja timu hizo katika kikao cha chama cha mpira wa
miguu wila ya Ludewa(LUDIFA)katibu wa chama hicho Bw.Mvanginyi alisema timu
hizo ni Home boys ,Polisi Ludewa,National ya Lugarawa na Kurugenzi ya Ludewa
nyingine ambayo haijathibitisha ni Lake star ya Manda.
Mvanginyi alisema timu nyingine zinazobaki zitashiriki
katika rigi daraja la tatu na zitakazo shinda timu nne zitaungana kukipiga rigi
daraja la pili mwakani.
No comments:
Post a Comment