Wanakikundi cha ufugaji wa n g’ombe wa kijiji cha Kiyogo
kata ya Masasi wilayani Ludewa wamenufaika na kikundi hicho baada ya kupata
fedha katika mradi wa TASAF ambayo iliwanufaisha kwa kuwanunua Ng’ombe na
kuwafuga.
Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa kikundi hicho
Bw.John Yahaya alisema mradi wa TASAF uliwapatia fedha shilingi million nane na
laki tano ambazo ziliwawezesha kuwanunua Ng’ombe tisa na ujenzi wa banda la
kuwafugia Ng’ombe hao.
Bw.Yahaya alisema kikundi chao kina wanachama kumi na tisa
ambapo kuna wanaume saba na wanawake kumi na mbili ambapo hugawana ndama na
mzunguko au mgao wa kwanza umeshakalika kwa kila mwanakikundi kupata ndama
mmoja.
Alisema wakati wanauanza mradi huo kuna wengi waliwakatisha
tama lakini kwa sasa kila mmoja wao ameweza kuona faida ya mradi hupo wenye
miaka mingi na unaowanufaisha bila kujali jinsia ya mwanakikundi katika mgao wa
ndama hao.
“Tumeanza kuona faida ingawa katika maeneo ya
Afya,barabra,elimu na maji safi na salama Serikali yetu imetususa lakini kwa
upande wa ufugaji ndio nguzo ya maisha yetu ya kila siku mpaka vijiji vya
jirani wanauonea wivu mradi huo”,alisema bwana Yahaya.
Aidha katibu wa kikundi hicho Bw.John Likwava alilalamikia
baadhi ya wanakikundi kushindwa kutimiza wajibu zao katika zamu za kuwachunga
ng’ombe hao hali ambayo inapelekea ngo’mbe hao kuwa na Afya mbovu.
Bw.Likwava alisema utaratibu ulikuwa kila mwanakikundi hata
kama ni mzee lazima apangiwe zamu ya kuwapeleka ng’ombe malishoni ambapo kila
mmoja atafanya kazi hiyo kwa muda wa wiki moja lakini kuna watu ambao
wanaonesha dalili mbaya.
Alisema kama wanakikundi watashiriki kikamilifu katika
utunzaji huo wa mifugo basi kikundi chao kitapata mafanikio makubwa kwani
wanampango wa kuwauza ng’ombe waliozeeka ili waanzishe mradi wa mashine ya
kusaga nafaka.
Alisema kumekuwa na changamoto za hapa na pale katika
kuwafuga ng’ombe hao ikiwemo ukosefu wa madawa ya kuwatibu ng’ombe hao na
kuwaogeshea kutokana na umbali wa maduka ya dawa za mifugo na uchumi duni wa
wanakikundi.
Bw.Yahaya alitoa sifa kubwa katika mradi wa TASAF kwa
kuwakumbuka wananchi wa vijijini kushinda miradi mingine inayoendeshwa na
Serikali kutokana na umbali wa kijiji na wataalamu wa TASAF waliolazimika
kutembea kwa miguu zaidi ya kilomita 15 kufika kijijini hapo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment